IDARA YA UTAWALA NA RASILIMALI WATU
UTANGULIZI:
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ina jumla ya Tarafa 6, Kata 28, Vijiji 133, Vitongoji 747, Idara13, Vitengo6 na majimbo mawili (2) ya Uchaguzi ambayo ni Kalenga na Ismani.
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ina jumla ya watumishi 3287. Idadi hiyo ni watumishi waliopo Makao Makuu ya Halmashauri na sehemu za kutolea huduma kama Hospitali , Zahanati , Shule , Ofisi za Kata na vijiji.
IDARA YA UTAWALA NA RASILIMALI WATU:
Idara ya Utawala ni kiunganisho kikuu cha Idara zingine, Idara hii ina jumla ya watumishi 220.Watumishi wa idara hii ni pamoja na Mkurugezi Mtendaji (W), Maafisa Utumishi, Makatibu wa Kamati, Makatibu Muhtasi, Madereva ,Walinzi ,Watunza Kumbukumbu, Wasaidizi wa Ofisi , Watendaji wa Kata na Watendaji wa Vijji.
Majukumu ya Idara ya Utumishi
NB. HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA INA MAZINGIRA MAZURI NA WEZESHI KWA MTUMISHI KUFANYA KAZI KWA UFANISI NA KUPELEKEA MTUMISHI HUYO KUYAFIKIA MALENGO BINAFSI IKIWEMO UJENZI WA MAKAZI BINAFSI KUJIENDELEZA KIMASOMO NA SHUGHULI ZA KIUCHUMI.
KARIBUNI SANA IRINGA
Mtaa wa Gangilonga
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0767778106
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa