• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe Za Watumishi |
Iringa District Council
Iringa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu sekondari
      • Elimu Msingi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo umwagiliaji na ushirika
      • Mazingira na Usafishaji
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA NA Uhusiano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipango,Utawala na Uchumi
      • UKIMWI
      • Afya Elimu na Maji
      • UMazingira, uchumi na Ujenzi
      • Maadili
    • Ratiba Ya Vikao mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Hudumakwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video za Shughuli Mbalimbali za kiofisi na za Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi 20,000 kuondokana na adha ya maji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Imewekwa : April 17th, 2018


Wananchi zaidi ya 20,000 wa Vijiji vya Magombwe,Isele,Kinyika na Kisanga wataondokana na adha ya maji mara baada ya Miradi miwili ya upanuzi wa Mradi wa maji Pawaga kwenda vijiji vinne Kata ya Mlenge kukamilika.

Akiongea wakati wa hafla ya utiaji sahihi wa Mikataba miwili ya Upanuzi wa Mradi wa maji Pawaga kwenda Vijiji vine vya Kata ya Mlenge, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw.Robert Masunya amewataka Wakandarasi waliochaguliwa kutekeleza Miradi hii miwili ya maji kufanya kazi kwa uadilifu na kuachana na masuala mengine ambayo yatakwamisha kutekeleza Miradi hii kwa wakati huku akiwakumbusha kuwa wanalo jukumu kubwa kuhakikisha kuwa Miradi inayotekelezwa inajengwa kwa ubora unaoelezwa katika mikataba iliyosainiwa.

Pia  amewataka kukamilisha Miradi hii katika muda wa mkataba ili uanze kutoa huduma kwa wananchi mapema ili kuleta maendeleo yanayohitajika na wananchi.

Aidha ameonya suala la rushwa lisiingizwe katika kazi, ‘’Mimi siamini kama tunaishi kwa rushwa,nimesimamia Miradi mikubwa ya maji ukerewe bilioni 13, Miradi ya Sengerema bilioni 21, kwa hiyo siyo kwamba hiyo bilioni 4 kwangu itanipa shida naona ni kitu cha kawaida tu,na haitaniondolea uimara wangu,mimi nitasimamia Miradi hii kwa uimara na kuhakikisha inatoa matokeo makubwa’’. Alisema  Bw. Masunya.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe.Steven Mhapa amewataka Wakandarasi waliochaguliwa kutekeleza Miradi hii kufanya kazi kwa ufanisi na uaminifu mkubwa na kampuni itakayoshindwa  kufanya kazi katika ubora unaotakiwa hatasita kutoiruhusu kufanya kazi ndani ya Halmashauri yake.

Mh.Mhapa pia amewataka wakandarasi washirikiane na wananchi katika ngazi za kata na vijiji ili kuhakikisha ushiriki wa wananchi katika Miradi inayowazunguka.

Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imesaini Mikataba miwili ya upanuzi wa Mradi wa maji yenye thamani ya shilingi bilioni 4.8,Mikataba hiyo ni Upanuzi wa Mradi wa maji Pawaga kwenda vijiji vine vya kata ya Mlenge,kujenga mabomba ya kusambaza maji kwenda Magombwe, Isele, Kinyika na Kisanga chini ya Mkandarasi GNMS Contractors LTD wa S.L.P 107 Iringa kazi hii itagharimu shilingi bilioni 3,216,845,931 na itatekelezwa kwa muda wa miezi 18.

Na Mkataba wa pili ni Upanuzi wa Mradi wa Maji pawaga kwenda vijiji vine vya Kata ya Mlenge,Ujenzi njia kuu mpya ya usambazaji 14.6km kutoka tanki la maji masafi kwenda kwenye tanki la luganga na Magozi, kutengeneza kituo cha kusafishia maji,tanki Ilolompya 50m3, Kimande 75m3 na Mbuyuni chini ya Mkandarasi M/S HEMATEC INVESTMENT LTD wa S.L.P 34078 Dar-es-salaaam,kazi hii itagharimu shilingi bilioni 1,647,262,810 na itatekelezwa kwa muda wa miezi 12.

Matangazo

  • Taarifa kwa Umma. April 16, 2018
  • Tangazo la Uhakiki wa vyeti March 07, 2018
  • Tangazo la ujio wa Madaktari bingwa kutoka Ujerumani katika Kituo cha Afya Ifunda February 09, 2018
  • Kuhudhuria Baraza la wazi la Madiwani February 09, 2018
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Aliyoyasema Waziri wa Nishati Mh. Medard Kalemani wakati wa uzinduzi wa umeme wa Rea katika Kijiji cha Mibikimitali.

    April 20, 2018
  • Wananchi 20,000 kuondokana na adha ya maji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

    April 17, 2018
  • Kaya 8125 Zimenufaika na fedha za Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF).

    March 27, 2018
  • Kaya 8125 Zimenufaika na fedha za Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF).

    March 27, 2018
  • Tazama zote

Video

Msikilize Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw. Robert Masunya akitoa neno wakati wa utiaji sahihi wa Miradi miwili ya upanuzi wa miradi ya maji.
video

Viungo vya haraka

  • Dashibodi ya Mapato
  • Salary slip

Viungo vinavyohusiana

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais-Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais -Utumishi na Utawala Bora
  • Sekretariati ya ajira
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti kuu ya takwimu huria

Idadi ya watembeleaji duniani

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Gangilonga

    Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa

    Simu ya mezani: 026-2702828/2702585

    Simu ya mkononi: 0754 364 994

    Barua pepe: ded@iringadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Watembeleaji

https://bachelorthesiswritingservice.com

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa