2. 0 HALI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILIYOKAGULIWA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA MAY 2018
2.1 SEKTA YA ELIMU MSINGI
NA |
JINA LA MRADI |
MAHALI ULIPO |
HALI HALISI YA UTEKELEZAJI |
FEDHA ILIYOTOLEWA |
MATUMIZI HALISI |
BAKI |
MAONI |
2.1.1
|
Ujenzi wa madarasa matatu (3) na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Mkungugu.
|
Kijiji cha Mkungugu
|
Ujenzi wa madarasa 3 na ofisi 1 upo katika hatua ya umaliziaji (finishing). Kazi zinazoendelea kupiga plasta, kuweka milango, dari, kuweka sakafu na utengezaji wa madawati unaendelea. Utekelezaji umefika asilimia 85.
|
66,600,000 |
50,657,500 |
15,942,500 |
Timu ya Ukaguzi inashauri kasi ya ujenzi iongezwe ili ujenzi ukamilike haraka kulingana na muda uliotakiwa. Pia timu inashauri wahakikishe ujenzi unakamilika haraka kulingana na muda uliotakiwa. Aidha fedha ya ujenzi wa vyoo iliyoombwa kubadilisha matumizi ifuatiliwe ili itumike kukarabati madarasa mengine yaliyochakaa.
|
2.1.2
|
Ujenzi wa madarasa matatu (3) na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Mboliboli
|
Kijiji cha Mboliboli
|
Ujenzi wa madarasa 3 kuta zimeshainuliwa na kumiminwa bimu. Kazi zinazoendelea upigaji wa plasta, kumwaga jamvi la chini (zege) na ununuzi wa vifaa vya umaliziaji unaendelea. Ujenzi wa matundu 6 ya vyoo shimo limeshachimbwa, linatakiwa kufanyiwa marekebisho kulingana na BOQ. Utekelezaji umfikia asilimia 45.
|
66,600,000 |
22,790,000 |
43,810,000
|
Kutokana na mradi huu kasi yake kuonekana ndogo, timu ya ukaguzi inashauri Afisa Elimu Msingi (W) na Mhandsi wa ujenzi (W) wafanye ufuatliaji wa karibu kuhakikisha wanaongeza kasi ili ujenzi ukamilike kwa wakati kama ilivyotakiwa kwani bado wapo nyuma katika utekelezaji. Aidha fundi mkuu alishauriwa kuongeza idadi ya mafundi na vibarua ili waendelee na ujenzi wa matundu ya vyoo kama ilivyotakiwa.
|
2.1.3
|
Ujenzi wa madarasa matatu (3) na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Lyalamo
|
Kijiji cha Tosamaganga
|
Ujenzi wa madarasa 3 yameshapauliwa na kupigwa lipu nje na ndani, sakafu imeshawekwa na dari. Kazi zilizobaki kuweka madirisha, milango na hatua nyingine za umaliziaji. Ujenzi wa vyoo, kibanda kimeshapauliwa, kazi zinazoendelea kumalizia uchimbaji wa shimo. Utekelezaji umefikia asilimia 89.
|
66,600,000 |
48,139,200 |
18,460,800 |
Ujenzi wa matundu 6 ya vyoo utaunganishwa kwenye shimo la zamani kutokana na eneo kuwa dogo la ujenzi, hivyo timu ya ukaguzi imemshauri Mhandisi wa Ujenzi (W) na kamati ya ujenzi ya shule kama kutakuwa na kiasi kitakachobaki watengeneze miundombinu kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu kuweza kufika mahali choo kilipo. Pia timu ya ukaguzi inashauri kufanyike marekebisho kwenye sakafu zote zilizowekwa kwenye madarasa 3 kwani hakuna slope ya kuwezesha maji yatoke kirahisi na kusababisha maji kutuama.
|
2.1.4
|
Ujenzi wa madarasa matatu (3) na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Makota
|
Kijiji cha Makota
|
Ujenzi wa madarasa 3 kuta zimeshainuliwa na kumiminwa bimu. Ujenzi wa matundu 6 ya vyoo shimo limeshachimbwa. Utekelezaji umefikia asilimia 35
|
66,600,000 |
17,861,500 |
48,738,500 |
Wakati wa ukaguzi hakukuwa na kazi inayoendelea na pia mafundi hawakuwepo site. Kutokana na utekelezaji kuwa nyuma timu ya ukaguzi wa miradi imeshauri mafundi waongezwe, pia kwa wananchi wamefanya kazi kubwa ya uchimbaji shimo, ukusanyaji mawe na tofali, hivyo kuna uwezekano wa kiasi cha fedha kubakia na kuongeza idadi ya matundu mawili ya choo na kufikia matundu 8.
|
2.1.5
|
Ujenzi wa madarasa matatu (3) na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Msukanzi
|
Kijiji cha Tosamaganga
|
Ujenzi wa madarasa 3 yameshapauliwa na kupigwa lipu nje na ndani, sakafu imeshawekwa na dari. Kazi zilizobaki kuweka madirisha, milango na hatua nyingine za umaliziaji. Ujenzi wa vyoo matundu 6, kibanda kimeshapauliwa, kazi zinazoendelea kupiga lipu nje na ndani na hatua nyingine za umaliziaji. Utekelezaji umefikia asilimia 88.
|
66,600,000 |
56,497,400 |
10,102,600
|
Timu ya ukaguzi inashauri Mtendaji wa kijiji kuhakikisha wananchi wake wanamalizia uchimbaji wa shimo la choo kama ilivyotakiwa.
|
|
2.2 SEKTA YA ELIMU SEKONDARI |
|
|
|
|
||
2.2.1
|
Ukarabati wa Mabweni 8 na matundu 16 ya vyoo katika shule ya sekondari ya Wasichana Ifunda
|
Kijiji cha Ifunda
|
Mabweni 8, na Matundu 16 ya vyoo vya Wanafunzi yamekarabatiwa. Utekelezaji umefikia asilimia 100.
|
106,416,000 |
106,416,000 |
0 |
Zikipatikana fedha nyingine ufanyike ukarabati kwa kupaka baadhi ya kuta rangi ambazo zinaoneka rangi zake kufifia.
|
2.2.2
|
Ujenzi wa madarasa 3 na matundu ya vyoo 5 katika shule ya sekondari Kiwele
|
Kijiji cha Mfyome
|
Ujenzi wa Madarasa 3 upo katika hatua za mwisho za umaliziaji (finishing) kwa kupaka rangi, kuweka vioo vya madirisha na kutengeneza madawati. Ujenzi wa matundu 5 ya vyoo umekamilika. Utekelezaji umefikia asilimia 95
|
65,500,000 |
62,340,140 |
3,159,860 |
Timu ya ukaguzi inashauri Kamati ya Ujenzi kuongeza taa za kwenye madarasa yote matatu ziongezwe ili kuwepo na mwanga wa kutosha kwani kwa sasa kila darasa kumewekwa taa 3 zile ndogo.
|
2.2.3
|
Ujenzi wa Mabweni 2 ya wanafunzi katika shule ya sekondari Isimila.
|
Kijiji cha Kaning’ombe
|
Ujenzi upo katika hatua ya kupandisha kuta na shimo la choo limeshachimbwa. Utekelezaji umefikia asilimia 35.
|
150,000,000 |
37,154,385 |
112,845,615
|
Ufuatiliaji wa karibu ufanyike kwani kasi ya utekelezaji hairidhishi kulingisha na muda walioanza ujenzi na muda ulibakia hadi kukamilisha ujenzi.
|
|
2.3 SEKTA YA AFYA |
|
|
|
|
||
2.3.1
|
Ujenzi/Upanuzi wa kituo cha afya Idodi ambao unahusisha majengo matano (Nyumba ya Mtumishi, maabara, wodi ya kina mama, jengo la upasuaji na jengo kuhifadhia maiti)
|
Kijiji cha Idodi
|
|
400,000,000 |
180,158,780 |
219,841,220
|
Kasi ya ujenzi iongezwe ili umaliziaji wa ujenzi ukamilike kwa muda uliopangwa na kuanza kutoa huduma. Aidha Timu ya ukaguzi inashauri Kamati ya ujenzi kazi zinazoweza kufanyika kwa wakati mmoja ni vizuri zikafanyika kwa pamoja, Pia kuwa na “provisional” ya mfumo wa malipo wa GOTHOMIS.
|
|
2.4 SEKTA YA MAJI |
|
|
|
|
||
2.4.1
|
Ujenzi wa mradi wa maji kwa kufunga solar panel 8, ununuzi wa pump, ujenzi wa pump house & tank tower, ununuzi wa tank la maji lita 5000 na ujenzi wa vituoa vitatu vya kuchotea maji shule ya msingi Mlambalasi
|
Kijiji cha Kipera
|
Ujenzi wa mradi huu umekamila na maji yanatoka kwenye vituo vyote vya kuchotea maji. Utekelezaji umefikia asilimia 99.
|
68,503,000 |
0 |
68,503,000 |
|
2.4.2
|
Ujenzi wa mradi wa maji kwa kufunga ununuzi wa pump, ujenzi wa pump house & tank tower, ununuzi wa tank la maji lita 5000 na ujenzi wa vituo vitatu vya kuchotea maji shule ya msingi Kiponzero
|
Kijiji cha Kiponzero
|
Ujenzi wa mradi huu umekamilka na maji yanatoka kwenye vituo vyote vya kuchotea maji. Utekelezaji umefikia asilimia 99
|
Kuongeza kituo kimoja kwa ajili ya wananchi ili wasiende kuchota maji kwenye vituo vilivyopo kwa ajili ya wanafunzi.
|
|||
2.4.3
|
Ujenzi wa vinawia mikono (Hand washing facilities) 10 katika shule za msingi za Chamgogo, Kiponzero, Mlambalasi, Mboliboli, Magombwe, Isele, Luganga, Makuka, Itunundu na Kidamali.
|
Vijiji vya Chamgogo, Kiponzero, Mlambalasi, Mboliboli, Magombwe, Isele, Luganga, Makuka, Itunundu na Kidamali.
|
Ujenzi wa vinawia mkono 10 umekamili kwa ailimia 100.
|
3,000,000
|
3,000,000 |
0 |
Mradi unatumika
|
2.4.4
|
Ujenzi wa mradi wa maji Izazi-Mnadani
|
Kijiji cha Izazi na Mnadani
|
Kisima kimeshachimbwa, nyumba ya pampu imeshajengwa, ulazaji mabomba na kuyafukia umekamlika, vituo 18 vya kuchotea maji vmekamilika. Pia katika kitongoji cha Ihanyi kisima kimeshachimbwa (sio kwenye kandarasi hii), ujenzi pump house umekamilika. Kazi zilizobaki ni ufungaji wa pump ya umeme ambao unasubiri usambazaji wa umeme katika kijiji cha Izazi, umaliziaji wa tank la lita 100,000, kuweka umeme wa jua katika kisima kilichopo Ihanyi, kuweka tanki la lita 5000 na kufanya umaliziaji katika maneo mengine. Utkelezaji umefikia asilimia 85.
|
725,056,271.01
|
535,447,890.76 |
189,608,380.25 |
Kufanya manunuzi ya pampu haraka kwa kufuata taratibu zote kwani umeme umekwishafika hadi eneo lililochimbwa visima ili mradi huu uanze kutoa huduma kwa wananchi.
|
2.4.5
|
Ujenzi wa mradi wa maji Migoli-Mtera
|
Kijiji cha Migoli na Mtera
|
Kisima kimeshachimbwa, pump house imeshajengwa, ulazaji mabomba na kuyafukia umekamlika, vituoa 20 vya kuchotea maji umekamilika na kufukia bomba kwa zege kwa maeneo yenye makorongo umefanyika. Pia katika soko la Migoli kisima kimechimbwa, ujenzi wa nyumba ya pampu umekamilika, pump ya umeme imefungwa, tanki la lita 5000 limewekwa na maji yanatoka. Aidha, kwa upande wa Mwanyengo umefanyika ujenzi wa pump house, uwekaji wa ‘solar pannel’ 8, kufunga pump controller na kufanya maboresho mengine. Kazi zilizobaki ni ufungaji wa pump ya umeme ambao unasubiri usambazaji wa umeme katika kijiji cha Izazi na kufanya umaliziaji katika maneo mengine. Utekelezaji umefikia asilimia 90.
|
1,385,930,662.02
|
979,091,560.92 |
410,839,101.10 |
Katika ukaguzi huo timu ilibaini kuwepo kwa makorongo mengine ambayo awali survey ilipofanyi kahayakuwepo. Hivyo timu ya ukaguzi inashauri Mhandisi wa Maji (W) katika eneo hilo mabomba yafukiwe kwa kumiminwa zege katika makorongo yaliyojitokeza.
|
Jumla Kuu |
3,237,405,933.03 |
2,099,554,356.68 |
1,141,851,576.35 |
|
Naomba kuwasilisha.
Robert M. Masunya
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Iringa
Mtaa wa Gangilonga
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0767778106
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa