Halmashauri ya wilaya ya Iringa hadi kufikia Disemba 2014 ina jumla ya shule za awali 113, Elimu maalum 1, Shule za msingi 146 na Vituo vya ufundi stadi 2 kwa mchanganuo ufuatao:-
Mafanikio
Changamoto
Sekta ya Elimu ya Sekondari.
Halmashauri kupitia Sekta ya Elimu Sekondari imeendelea kutekeleza kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusimamia ujenzi wa maabara 84 za masomo ya Sayansi, ujenzi wa hosteli ya wasichana shule ya sekondari Kalenga, ujenzi wa Hosteli ya Wasichana hatua ya kwanza Shule ya Sekondari Dimitriusi, Kuwapokea wanafunzi wa kidato cha tano, kufanya ufuatiliaji wa Taaluma katika Shule za Sekondari 28 pamoja na kusimamia ukarabati wa karakana ya kufundishia masomo ya Ufundi katika Shule ya Sekondari Ifunda ufundi.
Kumalizia ujenzi wa maabara tatu za masomo ya Sayansi kwa kila shule
Halmashauri kupitia Idara ya Elimu sekondari imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa maabara 84 za masomo ya sayansi. Ambapo Maabara 37 zimekamilika kujengwa na ambazo zinatumika kwa masomo ya Kemia na Baiolojia, maabara 4 bado zipo katika hatua za mwanzo za ujenzi. Maabara 43 zipo katika hatua ya umaliziaji ikiwa ni pamoja na kupiga lipu kufunga milango na madirisha. Jumla kuu ya michango kwa ajili ya ujenzi wa maabara ni Tshs. 355,160,000
Ujenzi wa Hosteli ya wasichana shule ya sekondari Kalenga.
Halmashauri imefanikiwa kukamilisha Ujenzi wa Hosteli ya wasichana shule ya Sekondari Kalenga. Ujenzi umegharimu kiasi cha Tshs 258,000,000.00 mpaka kukamilika na inatumika. Hosteli hiyo ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 120.
Ujenzi wa Hosteli ya wasichana hatua ya kwanza shule ya sekondari Dimitrius.
Halmashauri imejenga Hostel moja ya wasichana katika Shule ya Sekondari Dimitrious. Ujenzi wa hatua ya kwanza wa Hostel hii umekamilika na umefikia hatua ya kupauliwa. Ujenzi huu wa Hostel umegharimu Jumla ya Tshs 70,000,000 na awamu ya pili ya kumalizia ujenzi utaendelea mwaka wa fedha 2015/2016.
Mapokezi ya wanafunzi wa Kidato cha Tano.
Idara ya Elimu Sekondari imepangiwa jumla ya wanafunzi 2389 wa Kidato cha tano katika Shule zake sita.
Idadi ya wanafunzi wa Kidato cha tano kwa 2014/2015 imeongezeka kutoka 1433 mpaka 2389 sawa na asilimia 156% ukilinganisha na idadi ya wanafunzi waliopokelewa mwaka 2013/2014. Ongezeko la idadi ya wanafunzi hao katika Shule za Sekondari za Halmashauri ya Wilaya ya Iringa linaonyesha namna Halmashauri inavyochangia kwa kiasi kikubwa kutoa nafasi za wanafunzi kupata elimu ya kidato cha sita.
Ufuatiliaji wa Maendeleo ya Taaluma katika Shule ya Sekondari za
Muhwana, Isimila, Kiwere na Ifunda Ufundi.
Halmashauri imefanya ufuatiliaji wa ufundishaji na Maendeleo ya Taaluma katika Shule za Sekondari 28 za Halmashauri yetu. Zoezi la ufuatiliaji limefanyika ili kuona hali halisi ya ufundishaji pamoja na matumizi ya fedha ya ruzuku. Baada ya zoezi hilo wakuu wa Shule hizo pamoja na walimu waliagizwa kusimamia vizuri matumizi ya fedha za Ruzuku pamoja na ufundishaji na ujifunzaji ili kuinua taaluma Shuleni.
Kusimamia ukarabati wa karakana ya kufundishia masomo ya ufundi katika shule ya Sekondari ya ufundi Ifunda.
Halmashauri imesimamia kufanyika kwa ukarabati wa karakana ya kufundishia masomo ya ufundi katika shule ya Sekondari ya ufundi Ifunda. Ukarabati huo upo katika hatua za mwisho na umegharimu Tsh 355,000,000.00
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa