TAARIFA YA BWAWA LA MTERA
Bwawa la Mtera lilitengenezwa kwa ajili ya kuhifadhi ya kufua umeme kwa ajili ya Bwawa la Kidatu na kuanza kazi mwaka 1981. Bwawa hili lina ukubwa kwa kilomita za mraba 660 na lipo katika eneo linalozunguka Halmashauri za wilaya za Chwamwino na Mpwapwa katika mkoa wa Dodoma na Halmashauri ya wilaya ya Iringa katika mkoa wa Iringa ambapo ina eneo la kilomita 220.
Eneo la Bwawa la Mtera katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa linajumuisha kata ya Migoli katika vijiji vya Kinyali, Mbweleli, Makatapora, Mtera, Migoli na Mapera. Kata ya Izazi pia imo katika eneo la bwawa hili katika vijiji vya Mnadani na Makuka. Uwepo wa Bwawa hili umekuwa na faida kwa wananchi kwan imewawezesha kufanya shughuli za uvuvi kutokana na uwepo wa aina mbalimbali za samaki kama Perege, Mchena, Katoga, Kambale, Sulusulu, Mkunga, Ngobero, Ndua, Ngogo, Mbapala, Ngogomawe, Justin, Dagaa msumari, Dagaa kamba, Pua, Ngalala na Kimbumbu.
Forodha au kambi rasmi 17 za uvuvi zipo katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kama ifuatavyo; Ladwa, Mbweleli, Makatapora, Chapuya, Changarawe, Mapropela, Mkungugu, Madafu, Vietnamu, Nyegele, Maperamengi, Mnadani, Mabati, Magungu, Kilambakitali, Itemagwe na Kastamu. Forodha hizo zina jumla ya wavuvi 1500 na mitumbwi 1126.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa