IDARA YA UTAWALA NA RASILIMALI WATU
Idara hii ina jumla ya watumishi 220. Watumishi wa Idara hii ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji (W),Maafisa Utumishi,Makatibu Muhtasi,Madereva,Walinzi,Wasaidizi wa Kumbukumbu,Wasaidizi wa Ofisi,Maafisa watendaji wa kata na Maafisa Watendaji wa vijiji.
MAJUKUMU YA IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI
Kushughulika na masuala yote ya utawala na uendeshaji wa ofisi
Kuhakiki taarifa za utekelezaji za robo, nusu na za mwaka za idara zinazohitajika kwenye vikao, Tume ya Utumishi wa Umma, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na kwingineko
Kushughulikia masuala ya itifaki na mapokezi ya wageni
Kusimamia utendaji wa kazi wa ngazi za chini, kata, vijiji na vitongoji
Kushughulikia mikataba ya huduma kwa mteja
Kushughulikia uhamisho wa watumishi
Kushugulikia masuala ya nidhamu: Kushauri hatua zinazostahili kwa watumishi wenye makosa mbalimbali ya kiutumishi kulingana na Kanuni za utumishi wa umma
Kuratibu maandalizi ya bajeti ya mishahara ya watumishi wote na matumizi mengineyo kwa idara ya utawala na Utumishi.
Kushughulikia masuala yote ya Utawala Bora likiwemo na suala la masanduku ya maoni katika ngazi za Halmashauri, kata, vijiji na vitongoji na kuhakikisha kuwa maoni hayo yanafanyiwa kazi na kurudisha mrejesho kwa wakati
Kushughulikia matukio mbalimbali katika Halmashauri ikiwemo Vifo, Ajali, nk
Kushughulikia matatizo na migogoro inayotokana na mikutano ya Halmashauri, Kata, vijiji na vitongoji
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa