RC-Iringa sitowaacha salama wabakaji,walawiti katika Mkoa wa Iringa.
Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa -DC)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh.Queen Sendiga ameliagiza jeshi la polisi mkoani hapa kulipa kipaumbele suala la upelelezi wa kesi za ubakaji,ulawiti na ukatili wa kijinsia unaofanywa katika maeneo mbalimbli ndani ya mkoa wake.
Mh.Sendiga alitoa kauli hiyo wakati wa kuhitimisha ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambapo mbali na kukagua miradi pia alisikiliza kero za wananchi katika Kijiji cha Igingilanyi Kata ya Kising’a Agosti 17/2021.
Alisema “Inashangaza na kusikitisha mkoa wetu pamoja kuwa katika orodha ya mikoa yenye idadi kubwa ya wananchi wenye utapia mlo lakini pia kumekuwa na matukio ya ukatili ikiwemo ubakaji na ulawiti suala ambalo siko tayari kulifumbia macho na hapa na sisi nina kuagiza Mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Juma Mbwile kuwajulisha wapepelezi wako kulipa uzito suala la upelelezi wa makosa haya ya ubakaji na ulawiti” nakuongeza;
“Askari Kata nawaagiza kuwachukulia hatua wananchi wote ambao wanajishughulisha na biashara ya uuzaji wa pombe (vilabu) na wanafungua vilabu hivyo kabla ya muda uliopangwa kisheria lakini pia wananchi ama wakina mama watakaokuwa wanaenda na watoto ama kuwatuma Watoto kununua vileo na sigara alisema.
Aidha,akizungumza na wananchi Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Mohamed Hassain Moyo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi kutosikiliza uvumi na upotoshaji unaoenezwa na watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii kuhusu chanjo ya UVIKO 19 (COVID-19) kwa kuwa wanayozungumza sio sahihi.
“Tarehe mosi mwezi Septemba nitakuwa na ziara ya kusikiliza kero ya Kijiji kwa Kijiji ambapo nitaambatana na wataalam mbalimbali na kwa yeyote atakayekuwa tayari kwa hiyari yake na sisitiza chanjo hii ni hiyari ataweza kuchanjwa kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba”alisema.
Mh.Moyo alitoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kueleza kero na changamoto zao ili aweze kuzipatia uvumbuzi kwa kuwa lengo kuu la serikali ni kuwatumikia wananchi na kuziondoa kero na changamoto zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw.Bashir Muhoja aliahidi kuzifuatilia kero na changamoto za wananchi ambazo Mkuu wa Mkoa alimtaka kuzishughulikia na kumpa mrejesho kwa wakati kero hizo ni pamoja na mwananchi aliyedai kuzuiwa kutumia shamba la marehemu baba yake,kuorodheshwa majina ili kupatiwa huduma ya maji bila huduma hiyo kufika kwa takribani mwaka mmoja,kuibuka kwa ujenzi holela wa nyumba za ibada ambazo baadhi yake zimekuwa zikiknzana na sheria,kanuni na taratibu kwa kutumia vipasa sauti vikali na kuwa kero kwa wakazi wa maeneo hayo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa