MBUNGE MH MWAMWINDI ATOA SARUJI MIFUKO 60 HALMASHAURI YA IRINGA.
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano Iringa DC)
Mbunge Viti Maalum kupitia Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh Zainabu Mwamwindi leo Mei 5 amekabidhi mifuko 60 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambayo imeelekezwa katika sekta ya Afya na Elimu.
Mh Mwamwindi alisema ametoa mifuko hiyo ili kuisaidia Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika kuboresha Miundombinu ya Shule za Kalenga na Lupembelwasenga pamoja na Zahanati ya Ihominyi iliyopo katika Kata ya Kihorogota.
Alisema Saruji hiyo amepewa na Shirika la Nyumba la Taifa baada ya kupokea maombi kutoka katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hususani vijijini kwani Mvua kubwa zilizonyesha mwaka huu zimeharibu Miundombinu mingi sana.
“Mwaka huu Mvua zilikuwa nyingi sana na zimenyesha kwa kipindi kirefu hivyo kuna baadhi ya maeneo Miundombinu imeharibiwa vibaya sana lakini kwa kipindi hiki ambacho shule zimefungwa nimeona nielekeze mifuko 40 ya Saruji Shule ya Msingi Kalenga na 10 Shule ya Lupembelwasenga ili wanafunzi wakianza kusoma wakute Miundombinu imeshaimarika”alisema.
Akipokea Saruji hiyo kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw Peter Fussi ambaye ni Afisa Elimu Wilaya ya Iringa alisema “Mkurugenzi ameshukuru sana kwa kupokea Saruji hii na kuomba usichoke kutusaidia katika Idara mbalimbali ili kuboresha huduma kwa wananchi wetu ambao wanaitegemea Serikali yao kwa asilimia kubwa”.
Alisema “Kupokea Saruji hii ni neema kwa kuwa wahitaji na mahitaji ni mengi lakini Mh Mwamwindi umetuteua sisi Halmashauri tunakushukuru sana sana, kwani eneo ulilolielekeza kutoa saruji lina uhitaji mkubwa.”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa