Wakina baba watakiwa kuhudhuria Kliniki.
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano)
Rai imetolewa kwa wakina baba ya kuhudhuria Kliniki na wake zao ili kufahamu masuala muhimu ya lishe na ukuaji wa mtoto ili kuondokana na janga la utapia mlo na udumavu katika jamii zao.
Hayo yamezungumzwa na Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika kikao cha Kamati ya lishe kilichofanyika leo katika ofisi za Halmashauri.
Akizungumza katika kikao hiko, Afisa Lishe wa Wilaya Bi.Tiliza Mbula amesema kuwa bado kumekuwa na mwitikio mdogo wa utumiaji wa vidonge vya kuongeza wekundu wa damu katika jamii vidonge ambavyo vina Folic Acid na Madini chuma.
“Pamoja na jamii kupewa vidonge hivi katika vituo vya Afya na Zahanati lakini wamekuwa wakivitupa kwa kushawishiana wanapokuwa katika vikundi kuwa vina leta kichefu chefu”
Alisema na kuongeza kuwa
“Niombe wakina baba wawapeleke wake zao kliniki ili waweze kuwasimamia wakati wa matumizi ya dawa hizi kwani zinapelekea kupata matokeo mazuri ya kizazi chenye tija ambacho kinaanza kujengwa siku elfu moja (1000) tangu mimba kutungwa”alisema.
Moja ya matokeo mabaya ya kutotumia vidonge vya kuongeza wekundu wa damu ni pamoja n kuzaliwa watoto wenye vichwa vukubwa au kuzaliwa mgongo wazi,hivyo wakina mama wanashauriwa kuwahi Kliniki mapema ili kumlinda mtoto ambae atazaliwa.
Kwa Upande wake Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Dkt.Samuel Marwa amesisitiza juu ya uchukuaji wa Tahadhali ya ugonjwa wa Covid 19 unasababishwa na virusi vya Corona amesema iwapo mama atakuwa na maambukizi hayo anaweza kumnyonyesha mtoto kwa kutumia titi lake iwapo halitakuwa na wadudu.
Mama atakayebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona hatonyenyesha moja kwa moja ili kumkinga mtoto na maambukizi badala yake,mtoto atakuwa ana kunywa maziwa kupitia chupa maalum za kunywea maziwa watoto au kikobe.
“Nasisitiza jamii kuendelea kutoa ushirikiano pindi waonapo mtu ana dalili za ugonjwa huu lakini pia kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia kitakasa mkono mara kwa mara na uvaaji wa barakoa kwani hii itakusaidia kukukinga wewe na jamii inayokuzunguka”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa