Mafunzo Kuhusu Lishe na Sahani ya Mfano
“Tunapojifunza kuhusu sahani ya mfano, tunachukua hatua kuelekea kubadilisha mtazamo wetu kuhusu lishe. Kupitia mafunzo haya, tunalenga kuwa na mbinu bora za kuwezesha mabadiliko katika tabia za lishe kwa wanafunzi wetu”.
Kauli hii imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Veronica Kessy alipokuwa anafungua mafunzo kuhusu Lishe na Sahani ya Mfano, ambayo yamefadhiliwa na Shirika la Asante Afrika kwa kushirikiana na Agri – Connect, ambapo ilikuwa Januari 18, 2024, kwa wanafunzi wa shule za Msingi za Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Kalenga iliyopo Kata ya Kalenga.
Mafunzo haya yamelenga kuwakumbusha Walimu, Wazazi/Walezi na wanafunzi jinsi wanavyotakiwa kufanya katika kuandaa mlo kamili kila siku.
Mheshimiwa Kessy ameendelea kusema kuwa, “Mafunzo haya ni fursa kubwa kwenu kujifunza mambo mapya. Jitahidini kuelewa na kuyatumia katika maisha yenu ya kila siku. Mkumbuke kuwa, mnayo nafasi kubwa ya kuchukua uongozi katika kuleta mabadiliko chanya katika familia zenu na jamii kwa ujumla”.
Naye Afisa Lishe Wilaya Bi. Tiliza Mbulla, amewashukuru Wadau mbalimbali wanaotambua umuhimu wa Lishe, Walimu na Wanafunzi walioshiriki mafunzo hayo na kuamini kuwa, mafunzo haya yataleta mabadiliko chanya katika mwelekeo wa lishe na afya ya wanafunzi wa shule zetu.
Naye Mratibu wa mafunzo hayo Bi.Florence Thomas John, aliweza kuwasilisha video fupi za mfano kwa wanafunzi hao ili waweze kujinza kupitia video.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa