Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa lapitisha kitabu cha rasimu cha hesabu za Halmashauri kwa mwaka 2023/2024 kwa ajili ya hatua zingine za ukaguzi. Zoezi hilo limefanyika katika kikao Maalumu kilichoketi Agosti 30, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri - Ihemi.
Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Steven Mhapa ambaye amepongeza kazi kubwa na nzuri zilizofanywa na wataalamu pamoja na kamati ya fedha na kusisitiza kuhusu viambatanisho vya nyaraka muhimu zinazohusiana na taarifa ili kuepuka masuala ya hoja zisizo na ulazima.
“Moja ya vitu muhimu sana ambavyo mkaguzi anavihitaji ni viambata (Supporting documents) lazima viwepo maana mkaguzi hawezi kukubali utetezi wa maneno bali mkaguzi anataka nyaraka ambayo inajieleza inayosapoti maelezo yako” amesema Mhe. Mhapa.
Kwa upande wake Afisa Usimamizi fedha kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa ndugu George ametoa pongezi kwa namna kitabu kulivyoandaliwa na kusema kwa sehemu kubwa ni kama kitabu kipo tayari kwa ajili ya kuwasilishwa ambapo kama kutakuwa na marekebisho ni kidogo tofauti na Halmashauri zingine.
Pamoja na mambo mengine waheshimiwa madiwani wametoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji na Menejimenti ya Halmashauri kwa ukusanyaji wa mapato kwa zaidi ya asilimia 92 sanjari na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2023/2024 pamoja na changamoto za mfumo wa malipo zilizokuwepo ambazo pia wameshauri kuwa changamoto hizo ziainishwe ili zijulikane.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa