Care International Waadhimisha Kilele Cha Siku ya Wakulima
Care Internatinal ni Shirika lisilo la Kiserikali ambalo husaidia wakulima na Wajasiriamali na kuwawezesha kazi za mikono na kuwatafutia masoko.
Wadau wa Care wamekuwa msaada mkubwa katika kuwawezesha wakulima kuwapa mafunzo ya namna ya kulima kwa tija na kupata Mazao mengi na kutoa ushauri.
Katika kutekeleza majukumu yao Care wameadhimisha Siku ya Mkulima kwa kwenda kukagua shamba darasa ambalo lilipandwa zao la soya kwa Mkulima na Mjasiriamali
Hafla ya Kilele cha Mkulima imefanyika Aprili 11, 2025 katika Kata ya Mgama Kijiji cha Mgama kwa kualika Wadau mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine na Mbeya, na Wadau wengine kutoka sehemu mbalimbali.
Akiongea katika sherehe hizo Bwana Habibu Robert Masanja Meneja wa Mradi wa Care amesema, katika kutimiza malengo ya mkulima tuliweka vigezo nane ambayo ni kama njia ya kumuongoza mkulima kuwa, kuwawezesha vikundi na Maafisa Ugani ili waweze kufanya kazi kwa pamoja, kufanya ufuatiliaji kile kilichofundisha, suala zima la lishe, suala la jinsia hasa mwanaume mwenye mtazamo chanya, kufuatilia akiba na mikopo kwa vikundi, kukabiliana na tabia ya nchi ili mkulima aweze kulima kulingana na wakati, kutafuta masoko na ushawishi kwa Wadau mbalimbali.
Pamoja na hayo lengo la Care ni kufikisha mashamba darasa 800 ndani ya miaka mitatu ili wakulima waweze kujifunza kwa ukaribu zaidi.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Iringa Mheshdimiwa Stephen Mhapa ambaye alikukwa Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo amesema, “Shughuli ya kuelimisha wananchi ni ya Serikali lakini Wadau hawa wa Care wamejitokeza kuja kutushika mkono, hivyo sisi kama Serikali ni muhimu tuwaunge mkono na kuwaonesha njia. Pia vikundi hivi nashauri waombe mkopo ili waweze kutimiza kazi zao za ujasiriamali kama kununua mashine za kukamulia mafuta ili kuepukana na kwenda mbali kwa ajili ya kupata huduma hiyo”.
Mheshimiwa Mhapa ameendelea kusema kuwa, “nawakumbusha wakulima kuendelea kufuata ushauri kupitia mashamba darasa ili tulime kwa tija na tuongeze uchumi”.
Wananchi wameishukuru Care kwa kuja katika kijiji chao kuwafundisha kilimo cha kisasa chenye tija, na kuahidi kufuata mafunzo na ushauri waliopata.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa