CMT Yafanya Ziara Kukagua Miradi Kwa Robo ya Kwanza, 2023/2024
Kamati ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, imefanya ziara kukagua miradi Oktoba 16, 2023 kwa Robo ya Kwanza Julai – Septemba, kwa Mwaka wa Fedha 2023/2023.
Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wakili Bashir Muhoja, imetembealea miradi iliyokamilika na ambayo bado haijakamilika na kuwa ujenzi wake bado unaendelea.
Miradi iliyotembelewa ni kama Shule ya Sekondari Lufita, Kata ya Luhota, ambapo inajengwa nyumba ya Watumishi (2 in 1), ambapo Serikali ya Rais Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan ilileta fedha kiasi cha Milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo. Hadi sasa zimetumika Milioni 69.186 na kwamba ujenzi wake umefikia asilimia 50. Ujenzi ulianza Septemba 05, 2023 na unategemewa kukamilika Oktoba 30, 2023.
Aidha Kamati iliweza kutembelea Shule ya Msingi Itagutwa katika Kata ya Kiwele. Shule hii ilipewa fedha kiasi cha Milioni 40 kwa ajili ya ukarabati wa madarasa manne. Ukarabati huo utaanza mara baada ya mchakato wa uzabuni kukamilika.
Vilevile Kamati iliweza kutembelea Shule ya Sekondari mpya ya Weru ambayo ipo Kata ya Ulanda. Shule hii imejengwa kwa mpango wa SEQUIP, wa kujenga shule ambazo unajenga shule mpya ili kupunguza umbali mrefu kwa wanafunzi. Shule hii itawasaidia wanafunzi wanaotarajia kuanza Kidato cha Kwanza 2024 wa Kijiji cha Kibebe, Mwambao, Weru na Lipalama ‘B’, ambapo mwanzo walikuwa wanapangwa kwenda shule ya Sekondari Kalenga. Kiasi cha Milioni 583.128 na hadi sasa kiasi cha Milioni 527.503 kimetumika kujenga shule hiyo yenye madarasa 8, Jengo la Utawala, Maabara 3 (Kemia, Fizikia na Baologia), vyoo vya Walimu na vyoo vya wanafunzi. Nguvu za wananchi wamechangia kiasi cha Milioni 2.230. Mradi ulianza Agosti, 2023 upo hatua za mwisho na umefikia asilimia 90.
Kamati pia iliweza kutembelea Shule ya Sekondari Tosamaganga ambapo kulikuwa na ujenzi wa Bweni lenye thamani ya Milioni 130, Madarasa 3 Milioni 75 na ujenzi wa vyoo Milioni 12. Ujenzi ulianza Juni, 2023 na umekamilika Agosti 23, 2023 kwa asilimia 100 kwani majengo yote yanatumika.
Shule ya Msingi Wenda iliyopo Kata ya Mseke, ambapo imepewa kiasi cha Shilingi Milioni 60 kwa ajili ya ukarabati wa madarasa matatu. Ukarabati utaanza mara moja baada ya mchakato wa uzabuni kukamilika.
Shule ya Msingi Tarajiwa ya Kilimahewa (Kibaoni) iliyopo Kata ya Ifunda, imejengwa kwa Mpango wa Boost. Kiasi cha Milioni 347.5 kimetumika kujenga shule hiyo ambapo ujenzi ulianza Juni 01, 2023. Majengo hayo yataanza kutumika Januari, 2024. Hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 98. Shule hii itasaidia kupunguza umbali mrefu wa watoto ambapo wanakwenda shule ya Msingi Kibaoni.
Kamati ilifanya hitimisho la ziara yake katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ifunda iliyopo Kata ya Ifunda. Hapo kulikuwa na ujenzi wa bweni, madarasa na vyoo kwa Mpango wa Barick. Ujenzi ulianza Juni 20, 2023 na umekamilikwa kwa asilimia 100 Septemba 2023, na majengo yote yanatumika.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa