CMT Yafanya Ziara kwa Robo ya Tatu Kukagua Miradi ya Maendeleo
Kamati ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, imefanya ziara kukagua miradi ya maendeleo kwa Robo ya Tatu Mwaka wa Fedha 2022/2023, ambapo imeongozwa na Kaimu Mkurugenzi Ndugu Exavery Luyagaza ambaye ni Afisa Mipango na Uratibu Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ambapo ziara imefanyika tarehe 09/05/2023.
Kamati hiyo imeweza kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri ikiwemo mradi wa Kinga Maji ambao unatekelezwa Kata ya Kising’a kijiji cha Ilambilole, unaofanywa na walengwa wanaosaidiwa na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kupewa ajira za muda. Mradi umefikia 95 %, kwani ulianza tarehe 01/03/2023 na ulipewa muda wa siku 60 tu.
Kamati pia imetembelea Kijiji cha Mangawe Kata ya Nyang’oro kwenye mradi wa utengenezaji wa barabara kwa njia ya kulima yenye urefu wa Kilometa 1.5, ambapo unatekelezwa na walengwa wa TASAF, na mradi umekamilika na kuanza kutumika.
Aidha, Kamati imeendelea kufanya ukaguzi wa miradi yake kwa kwenda kijiji cha Makuka Kata ya Izazi kwa kukagua mradi wa ujenzi wa Josho. Mradi huo unategemea kutumia kiasi cha fedha Shilingi Milioni Arobaini za Kitanzania (Tsh. 40,000,000/-) hadi kukamilika kwake. Mradi ulianza 19/03/2023 na unategemewa kukamilika 19/03/2023, mradi umefikia 50% Mradi huu umefadhiliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira (Sustainable Landscape Restoration – SLR).
Kamati pia imeweza kutembelea Kijiji cha Mnadani Kata ya Izazi kwenye mradi wa ufugaji ng’ombe watatu wa maziwa. Mradi huu unatekelezwa na kikundi cha Tumsifu ambacho ni Watu Wenye Ulemavu ambapo wapo 6, Wanaume 4 na Wanawake 2. Mradi huu ulianza 10/03/2023. Ng’ombe mmoja anategemewa kutoa maziwa lita 15 – 20 akishaanza uzalishaji.
Kadhalika Kamati imetembelea Kijiji cha Migoli kwenye mradi wa upandaji miti ya matunda, ambapo kuna miti ya malimao, machungwa, mapera na maembe. Mradi huu pia unatekelezwa na walengwa wa TASAF.
Katika Kata hiyo ya Migoli Kijiji cha Makatapola kuna mradi wa ufugaji mbuzi 95, ambao unatekelezwa na kikundi cha Nanyorai ambapo wapo 20, Wanawake 17 na Wanaume 3.
Pia Kijiji cha Mbweleli kwenye mradi wa utengenezaji barabara kwa njia ya kulima, ambao unatekelezwa na walengwa wa TASAF. Barabara hiyo ina urefu wa Kilometa 1 na imeanza kutumika, ilipewa muda wa siku 60 tu za matengenezo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa