Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James amefanya ziara yake katika Tarafa ya Mlolo Mei 20, 2025 kama mwendelezo wa ziara zake za kijiji kwa kijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Akiwa Mlolo Mhe. Kheri ametembelea mradi wa maji kijiji cha Itwaga na ukarabati wa zahanati kisha mkutano wa hadhara ambao umefanyika kijijini hapo viwanja vya ofisi ya kijiji cha Itwaga kwa kuongea na wananchi sambamba na kusikiliza kero zao kisha kuzitafutia utatuzi.
Maeneo mengine ni vijiji vya Ihemi na wenda ambapo pia amefanikiwa kufanya mikutano ya wananchi kuwahamasisha katika kushiriki shughuli za kujiletea maendeleo na kusikiliza kero zao.
Katika ziara hii vilevile Mhe. Kheri ameweka msisitizo juu ya wananchi kutumza amani hasa wakati huu tunapoendelea na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu hapo mwezi Oktoba 2025 kwani fujo wakati wa uchaguzi inaweza kuathiri shughuli za kiuchumu na hata kuumiza wale wasio na uwezo yaani wazee watoto na akinamama.
#iringaimaratutaijengakwaumojanauwajibikaji
@ikulu_mawasiliano @ortamisemi @msemajimkuuwaserikali @iringarc @iringa_district @ndg.kheri_james @am_54masunya_r
https://www.instagram.com/p/DJ6TGI-M48-/?igsh=MXU0d2Uyb29tOXh5cw==
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa