Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Benjamin Sitta amepokelewa na kukabidhiwa ofisi mapema baada ya zoezi la uapisho kufanyika Juni 30, 2025. Mapokezi na makabidhiano hayo yamefanywa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wakuu wa vyombo vya usalama ngazi ya Wilaya, viongozi wa taasisi na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya na Manispaa wameshiriki mapokezi na kushuhudia makabidhiano hayo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa