Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Benjamin Sitta amewaasa wananchi kuishi kwa upendo kwani hawapaswi kuhasimiana wao kwa wao na kuwakumbusha kuwa adui yao ni umaskini.
Mhe. Sitta ameyasema hayo alipokuwa katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ilambilole kata ya Kising’a kusikiliza na kutatua kero za wananchi ikiwemo suala la uongozi Oktoba 09, 2025.
“Adui yatu ni umaskini, adui yetu sisi si wenzetu tukiongeza maarifa, juhudi, tukashiriki vikao, wale wenye ubunifu wanakuja nao, tutumie nguvu na akili kujiinua kiuchumi tukimtanguliza Mungu mbele” amesema Mhe. Sitta.
Aidha Mhe. Sitta amefanya ziara kukagua miradi ya maendeleo katika Kijiji cha Migoli kukagua hali ya stendi ya Migoli, kuona changamoto za stendi kutofanya kazi na kushauri mambo ya kufanya ili eneo lile lilete tija ya kimapato.
Pia mamekagua ukarabati wa Zahanati ya Makatapola, shule ya msingi Makatapola na ujenzi wa miundombinu ya madarasa katika shule ya msingi Makuka. Mhe. Sitta ametoa pongezi kwa uongozi wa uongozi wa shule ya msingi Makuka kwa kuendelea kufanya vizuri licha ya changamoto ya uhaba wa walimu
Mkuu wa Wilaya katika ziara yake ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ndg. Robert Masunya na wataalamu kutoka katika Idara na vitengo mbalimbali ili kutoa ufafanuzi na usaidizi juu ya masuala mbalimbali wakati wa ziara.
Kwa upande wao wananchi wa maeneo yaliyotembelewa wametoa shukrani na pongezi kwa Mkuu wa Wilaya kutembelea na kutatua changamoto mbalimbali.
#kurayakohakiyakojitokezekupigakura







Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa