DC Kheri James Ahimiza Ushiriki wa Vijana Katika Michezo
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James amewahimiza vijana kushiriki katika shguli za michezo ili kuimarisha afya, kujenga umoja, kupata burudani na kuifanya michezo kuwa njia nyingine ya kujiajiri kupitia vipaji walivyo navyo.
Mheshimiwa Kheri ameyasema hayo Mei 25, 2024 katika uzinduzi wa mashindano ya soka ya Sabasaba yanayoendelea katika Kata ya Ilolompya Tarafa ya Pawaga.
Pamoja na mambo mengine, Mheshimiwa Kheri ameeleza kuwa, Serikali itaendelea kujidhatiti kwa kushirikiana na Wadau, kuisimamia Sekta ya Michezo, kwa kuibua vipaji, kusimamia vipaji, kuimarisha miundombinu ya michezo na kukuza vipaji ili kuwa na wachezaji mahiri katika kila mchezo ili tasnia hii iendelee kuwa kimbilio la vijana wenye vipaji nchini.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa