DC Kheri Aipongeza World Vision kwa Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Kheri James ameungana na wananchi wa Kata ya Kihanga na Maboga kuadhimisha Siku ya Kilimo iliyofanyika katika Tarafa ya Kiponzero ambapo imeratibiwa na Shirika la World Vision.
Akizungumza katika Maadhimisho hayo Mheshimiwa Kheri amepongea Shirika la World Vision kwa kutoa mafunzo na mitaji kwa wananchi, kwa lengo la kuwajengea stadi za maisha na kuwawezesha kunufaika na rasilimali zilizowazunguka kuiuchumi.
Aidha Mheshimiwa Kheri amewahimiza wananchi kuendelea kulima kwa kuzingatia stadi za kilimo na ushauri wa Wataalamu ili kujipatia kipato na kupata uhakika wa chakula. Pia mavuno hayo kuyatumia kama chakula bora ili kupambana na udumavu na kuhakikisha familia zao zinakuwa na lishe bora.
Katika kufanikisha mpango wa kuimarisha mzunguko wa uchumi na kutengeneza uhakika wa soko la mazao ya wakulima, Mheshimiwa Kheri ameishauri Halmashauri kuwawezesha wakulima viwanda vidogo vya kuchakata mazao ili kuyaongezea thamani na wakulima waweze kuuza kwa bei nzuri.
Akizungumza kwa niaba ya Shirika la World Vision Meneja wa Kanda Bi. Pudensiana Rwezaura ameishukuru Serikali na wananchi wa Wilaya ya Iringa kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa katika mipango wanayoleta, na kuahidi kuimarisha ushirikiano huo ili kuendelea kusaidiana na jamii kuimarisha Sekta ya Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii.
Serikali katika Wilaya ya Iringa inaendelea kutambua mchango wa Wadau wa Maendeleo na inaahidi ushirikiano wa kutosha ili kuharakisha ustawi wa maendeleo ya wananchi.
“Iringa Imara, Tutaijenga kwa Umoja na Uwajibikaji”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa