Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri Denice James amepokelewa na viongozi mbalimbali akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica Kessy ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu alipowasili katika ofisi za Mkuu wa Wilaya zilizopo Mawelewele Manispaa ya Iringa mapema leo Machi 11, 2024
Akizungumza na Viongozi mbalimbali Mhe. Kheri James amesisitiza suala la watumishi na viongozi kufuata utaratibu katika utendaji kazi wao “Ili tuweze kuyafikia malengo ambayo Mhe. Rais anayatarajia, kila mmoja afanye nafasi yake mimi ni mtu wa utaratibu, naamini katika utaratibu, tutapendana kwenye utaratibu na tutapishana kwenye utaratibu” amesema Mhe. James.
Aidha, Mhe. Kheri amesisitiza juu ya mambo matano kwa viongozi wote ambayo ni; Utawala wa sharia, haki, usawa, maendeleo, umoja na mshikamano hivyo maamuzi yoyote ya viongozi lazima yajikite hapo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe. Steven Mhapa ametoa neno la ukaribisho kwa kusisitiza kuwa katika utendaji haki ni jambo muhimu na kwamba kila jambo linapaswa kufanyika kwa hekima na Mwenyezi Mungu ndiye anayetoa hekima.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa