DC Kheri James Awataka Watunza Kumbukumbu Kufanya Kazi kwa Uadilifu (TRAMPA)
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Kheri James amewataka Watunza Kumbumbuku kufanya kazi kwa uadilifu, kwani wapo katika kitengo maalumu cha kutunza nyaraka mbalimbali.
Ameyasema hayo alipokuwa anafungua kikao kazi cha Watunza Kumbukumbu hao kilichofanyika Mkoani Iringa Mei 07, 2024 katika Ukumbi wa Masiti uliopo Manispaa ya Iringa.
Mheshimiwa Kheri amesema, “Serikali inatambua na kuthamini sana mchango wa tasnia ya Menejimenti ya Kumbukumbu katika kuharakisha na kusaidia kufanya maamuzi sahihi na kwa haki na ustawi, pia kuwa waadilifu na kuzingatia maadili ya kazi”.
Aidha Mheshimiwa Kheri ameeleza kuwa, Serikali kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu Utumishi imeendelea kutoa maelekezo na miongozo ya namna bora ya utunzaji wa nyaraka.
Akitoa shukrani kwa niaba ya washiriki wa kikao hicho Mwenyekiti wa TRAMPA Bi. Devotha Mrope amewashukuru sana Waajiri kwa ujumla kwa kuendelea kuilea na kuisimamia vyema Kada hiyo muhimu katika Utumishi, na hivyo ameahidi kutumia kikao hicho kukumbushana misingi na wajibu ili kuongeza tija katika utendaji.
Kikao hicho kinatarajia kufanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia Mei 07 – 09, ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mheshimiwa George Simbachawene anatarajia kuhutubia na kuhairisha kikao hicho.
“Iringa Imara, Tutaijenga Kwa Umoja na Uwahibikaji”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa