DC Kheri James – “Matumizi Bora ya Fedha za Lishe Yataondoa Alama Nyekundu”
Kikao cha Mkataba wa Afua za Lishe Robo ya Kwanza kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 (Julai – Septemba), kimefanyika Novemba 21, 2024 ambapo kimeongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James, amesisitiza matumizi bora ya bajeti ya Afua za Lishe husaidia kuondoa alama nyekundu katika upimaji.
Mhe. Kheri ameyasema hayo alipokuwa anaongoza kikao hicho na kumsisitiza Mganga Mkuu wa Halmashauri na Mweka Hazina kufanya matumizi bora ya fedha hizo.
“kukiwa na matumizi bora ya fedha za lishe basi zinaweza kuondoa alama nyekundu katika upimaji wa afua za lishe, na hii itasaidia kuwa na asilimia zote katika utekelezaji wa afua za lishe”
Kabla ya kikao hicho kilitanguliwa na Kamati ya tathimini ya Mkataba wa Afua za lishe na kuona utekelezaji wake kwa kipindi cha robo ya Kwanza, pia kutoa taarifa ya utekelezaji kwa Idara zote zinazohusika katika suala la utekelezaji wa lishe.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa