Ahimiza umakini kwani mpango huu unaoandaliwa ndio unaotoa uelekeo wa Halmashauri na matumizi ya rasilimali
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Ndg. Robert Masunya amefungua kikao kazi cha wataalamu cha kuandaa Mpango Mkakati (Strategic Plan) wa Halmashauri unaotarajiwa kuanza 2026 hadi Juni 30, 2031.
Kikao hicho kinafanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo Iringa kuanzia tarehe 12 - 13 Novemba 2025 na kinawezeshwa na mtaalamu kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI - Hombolo) Ndg. Jonas Charles Kapwani.
Uandaaji wa Mpango Mkakati wa Halmashauri unaenda sambamba na tathmini ya kina ya Mpango Mkakati unaoishia 2025 ili kujua hali ya sasa na uelekeo mpya wa Halmashauri kufikia 2031.




Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa