Kutokuwajibika,Pombe vyaelezwa kuwa vyanzo vya matendo ya Kikatili katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Anton Ramadhan (Iringa - DC)
Kilele cha maadhimsho ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia ambapo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa yamefanyika katika Kata ya Magulilwa, Kijiji cha Ng’enza jana Disemba 3 mwaka huu wa 2021.
Akizungumza katika Maadhimisho hayo Diwani wa Kata ya Magulilwa Mh.Jane Mhangala ambaye alikuwa Mgeni Rasmi ametoa rai kwa wakazi wa Kata hiyo kujikita katika shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato ili kutopata muda wa kufanya matendo maaovu yakiwemo matendo hayo ya ukatili.
“Iwapo wananchi na Wakazi wa Ng’enza na Magulilwa kwa ujumla mkiwa mnatumia muda mwingi katika kazi za kuwaingizia kipato ni wakati gani mtapata muda wa kuwapiga,kuwang’ata,kuwachoma moto,kuwakatakata,kuwajeruhi au kubaka watoto”alisema na kuongeza
“Nina ahidi kwenda kuzungumza na taasisi inayojihusisha na masuala ya sheria ili waje kuwapa elimu ya sheria ili muweze kufahamu makosa na adhabu za mtu au watu wanaokinzana na sheria”alisema.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi.Gladness Amunike amewaomba wananchi kuwa wapesi kutoa taarifa za Ukatili kwa kuwa sasa katika maeneo yao wapo wananchi ambao wamefundishwa namna ya kutambua na kukabiliana na matendo ya ukatili wa kijinsia.
“Tusiwafiche wabakaji wa watoto wetu hata kama ni ndugu au wenza wetu tutoe taarifa haraka ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa na waliofanyiwa ukatili waweze kupatiwa msaada na huduma kwa haraka”alisema.
Aidha Kaimu Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Wilaya Bi Dora Mlomo amesisitiza umuhimu wa kujishughulisha na kazi mbalimbali za kijikwamua kiuchumi hasa kwa wanawake ili waweze kujizuia na matendo ya ukatili hasa ya vipigo na mashambulio ya mwili ikiwemo kuchoma moto watoto,kuwang’ata na kupata adhabu kandamizi.
Pia,Afisa Polisi Dawati la Jinsia na Watoto Elizabeth Swai ameelezea namna jamii inavyoharibu mashauri yakiwa katika hatua za awali za upelelezi,huku pombe ikitajwa kichochea kikuu cha matendo ya ukatili.
Amesema katika hatua za awali ndipo jamii iliyotendewa kosa hukuatana na upande wa mtenda kosa na kukubaliana kumaliza shauri hilo kwa kupeana fedha au mali na kupelekea mashauri mengi kutofanikiwa katika hatua ya maamuzi kwa kuwa jamii iliyotendewa kusita kufika mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi pindi wanapotakiwa kufanya hivyo au kuwatorosha wahusika waliofanyiwa vitendo vya kikatili.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa