Dkt. Kaijage Aipongeza Awamu ya Sita kwa Kuwajali Watumishi
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imetembelewa na Mbunge anayesemea wafanyakazi na kutetea maslahi ya watumishi Bungeni Dkt. Alice Kaijage Septemba 15, 2023
Mheshimiwa Dkt. Kaijage katika ziara yake ameweza kusikiliza kero mbalimblai za watumishi na kwenda kuzisemea Bungeni. Aidha Mheshimiwa Dkt. Kaijage anaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutatua baadhi ya kero za watumishi kwa kuwapandisha vyeo na madaraja mbalimbali.
Mheshimiwa Dkt. Kaijage amesema “katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali ilitenga bajeti kwa ajili ya kuwapindisha vyeo watumishi 12,000, na pia imeweza kuwabadilisha Kada (Muundo) watumishi mbalimbali na kiasi cha Shilingi Bilioni 2.5 zimetumika”.
Pia Mheshimiwa Dkt. Kaijage amefafanua juu ya suala la ajira na kwamba tangu Mheshimiwa Dkt. Rais Samia suluhu Hassan amiengia madarakani ameweza kutoa ajira katika nafasi mbalimbali zaidi 47,374 na bado ataendelea kutoa nfasi za ajira kwa Watanzani. Mwaka wa Fedha 2023/2024 Serikali imetenga nafasi za ajira 27,000 za nafasi mbalimbali.
Mheshimiwa Dkt. Kaijage amewaomba watumishi kuwa na Imani ya kufanya kazi kwa uadilifu na kuiombea Amani nchi ya Tanzani.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja aliweza kutoa ufafanuzi wa mambo kadhaa ambayo yalitolewa kama hoja na baadhi ya watumishi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa