Dkt. Mpango Atoa Maagizo Mazito Uhifadhi Mto Ruaha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ametoa maagizo mazito kwa wahusika wote wanaohusika kutunza na kuhifadhi mto Ruaha kuhakikisha wanatatua na kumaliza changamoto zinazoukabili mto huo ambao umekumbwa na ukame kutokana na sababu mbalimbali.
Dkt. Mpango ameyasema hayo katika Kongamano la Wahariri, na Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na Utunzaji wa Vyanzo vya Maji lililofanyika Desemba 19, 2022 Mkoani Iringa katika Ukumbi wa Masiti Grand ambapo alikuwa mgeni rasmi wa kongamano hilo.
Aidha Dkt. Mpango amesema kuwa “natoa maagizo na msisitizo kuwa, waandishi ni nguzo muhimu katika uendeshaji wa kampeni mbalimbali, kwa hiyo endeleeni kuhamasisha jamii juu ya kutunza mazingira, na Taasisi zote za Serikali zishirikishwe.
Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (Media Center for Information and Resources Advocacy – MECIRA) likiwa na lengo la kutafuta suluhu kutokana na uharibifu wa vyanzo vya mito na uhifadhi wa mazingira katika Mto Ruaha ambao umeharibiwa vibaya na kushindwa kutiririsha maji na kusababisha ukame.
Richa ya maagizo mbalimbli pia katika Hotuba yake Mhe Dkt. Mpango amewapongeza MECIRA, TEF na Wadau wengine kwa kuandaa Kongamano hilo, pia kufichua maeneo yaliyofanyiwa uharibifu na kutafuta suluhu ya jambo hilo.
Kila Kongamano na mikutano mbalimbali ya Wahabari lazima waweke mada za mazingira ili waweze kujadili juu ya uhifadhi mazingira. Pia kuwahamasisha Wahariri na Waandishi waandike habari za kuichunguzi katika Sekta ya Mazingira”.
Kadhalika Dkt. Mpango ameongeza kuwa Wanahabari lazima wapate elimu ya kutosha ya ekolojia ya mazingra, ndipo wataweza kuandika masuala ya mazingira na kupanda miti ya matunda, kivuli na dawa. Wakuu wa Mikoa wote nchini wawatumie Wakuu wa Taasisi na Wakurugenzi wa Majiji, Miji na Halmashauri za Wilaya kusimamia sheria ya mazingira. Pia elimu itolewe kuhusu usafi wa mazingira na kwamba uhifadhi uanze kwenye ngazi ya familia, shuleni na hata Taasisi za Dini.
Mheshimiwa Rais anahamasisha utalii kwa kuandaa filamu, (Royal Tour) na sasa itakuwa filamu ya Utalii Kusini ikijumuisha mbuga za Mikumi, Ruaha na Nyerere. Pia vyombo vya Habari vina mchango mkubwa sana katika kulitangaza Taifa.:
Mwisho Mheshimiwa Dkt. Mpango amemuagiza Waziri wa Mazingira kuandaa semina/mafunzo wezeshi kwa wanahabari juu ya utunzaji wa mazingira ifikapo Machi, 2023.
Mheshimiwa Dkt Mpango ameongeza kutoa maagizo kwa viongozi wa Mamlaka ya Mabonde ya Maji wachukue hatu sasa kwa wale walioziba mto Ruaha bila vibali sahihi na kwamba wabomoe kwa gharama zao wenyewe. Pia mamlaka ziandae Makala maalumu za mazingira, na Makala ya Kongamano hili na zirushwe kwenye Runinga mara kwa mara.
Aidha Dkt Mpango amewakumbusha Wizara ya Mifugo kuwa, kutoa mikakati ya kushughulikia changamoto, na watafute sehemu mbadala ya kufugia na kulishia mifugo na ifugwe kisasa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego ambaye ndiye alikuwa mwenyeji Mkoani hapo aliweza kuongea mambo mbalimbali kuwa, amemshukuru Mheshimiwa Rais, kwa kutoa fedha ili kutekeleza miradi mbalimbali inayoendelea Mkoani humo, ikiwemo fedha kwa ajili ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege, ujenzi wa skimu za umwagiliaji Kata ya Itunundu na Mboliboli – Pawaga, ujenzi wa madarasa, uboreshaji wa barabara, tani nyingi za mbolea ya ruzuku, umeme vijijini na kwamba Iringa inapiga hatua mbalimbali za maendeleo kwa ajili ya kutekeleza Ilani.
Aidha Mheshimiwa Dendego amesema wako tayari kunywa sumu na kusimama kidete kutetea mazingira ili kuondokana na ukame unaonyemelea Mkoa wa Iringa.
Mheshimiwa Dendego amemaliza kwa kusema kuwa, kama Mheshimiwa Rais ikimpendeza basi ipelekwe Kambi ya Jeshi ili kulinda eneo hilo la Mbuga.
Kongamano lilikuwa na maazimio mbalimbali na kupeana mikakati ya namna ya kuboresha na kulinda rasilimali hizi za mazingira.
Kongamano hili lilibebwa na kauli mbiu isemayo “Mazingira Yetu Uhai Wetu, Tuyalinde, Tuyatunze, Tuishi”.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa