Dkt. Msonde Afunga Mashindano ya SHIMISEMITA Dodoma
“Wakurugenzi hakikisheni watumishi wanashiriki mashindano ya michezo hii kikamilifu”
Kauli hii imetolewa Oktoba 30, 2023 na Naibu Katibu Mkuu – Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Charles Msonde alipokuwa akifunga mashindano ya michezo ya SHIMISEMITA, iliyoanza Oktoba 17, 2023 Jijini Dodoma.
Dkt. Msonde ametoa maagizo hayo pamoja na mengine kwa Wakurugenzi wote nchini kuwa, kutokana na mwakani kuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni wajibu wa kila Mkurugenzi kuelimisha wananchi kupitia michezo na mabonanza mbalimbali.
Aidha Dkt. Msonde ameendelea kutoa maagizo kwa kusema, Wakurugenzi wakati wa kuandaa bajeti, ni lazima kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya mashindano ya michezo hii, ili kuepuka kuwasumbua watumishi pale wanapokuja kushirki michezo. Ni vema michezo ikaanzia ngazi ya Kata hadi kufikia tamati kwenye Taifa.
Kdt. Msonde amewataka Wakurugenzi kuhakikisha kuwa, kati ya wau wanashiriki amshindanohayo wawe watumishi tu na siyo kuweka watu ambao siyo watumishi (mamluki), ili kuondoa sintofahamu kwa watu wengine na Kamatu ya maandalizi kwa ujumla
Pamoja na hayo Dkt. Msonde amewashukuru waandaji wa michezo hiyo, viongozis wa CCM, Madiwani na washiriki wote kweza kufanikisha mashindano hayo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa