“Dodoki ni kama ubongo wa mtoto mdogo ambaye anasoma na kujifunzi kila kitu, iwe kibaya au kizuri. Hivyo mtoto anatakiwa kujifunza mambo mazuri katika hatua za ukuaji wake”.
Kauli hii imtolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Stephen Mhapa alipokuwa anafunga mafunzo mafupi juu ya Uzinduzi wa Program ya Kitaifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT – MMMAM), katika Ukumbi wa Halmashauri uliopo Ihemi Februari 21, 2024.
Mheshimiwa Mhapa ameendelea kusema, “tunapaswa kuwatengeneza watoto wetu katika hatua tangu umri sifuri hadi miaka nane na ndiyo kipindi ambacho mtoto ananyonya na kujifunza mambo mengi mazuri na mabaya, kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa na Taifa safi la kesho”.
“Aidha, jambo hili ni mtambuka, haliwezi kufanyika na mtu mmoja tu, yatupasa kushirikiana ktika utekelezaji wake jamii na Wataalam tujifunze kupitia mpango huu”.
Mafunzo hayo yametolewa na Wakufunzi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa Bi. Grase Simalenga na Bwana Reuben Magayane kutoka IDYDC.
Mafunzo hayo yamelenga na kutambulisha Program hiyo ya MMMAM kwa ajili ya malezi na makuzi bora ya mtoto tangu kuanzia umri wa sifuri hadi miaka nane. Mpango huu ni jumuishi kwani unahusisha Kada za Elimu, Afya, Lishe, Ulinzi wa mtoto na uchangamshi kwa ujumla.
Baada ya uzinduzi maelekezo yametolewa kwa Wataalam wa Afya kupitia Kitengo cha Ustawi wa Jamii na Lishe kuandaa mpango kazi kwa ajili ya utekelezaji wake.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa