“Hadi Kufikia Machi 05, 2024, Walengwa wa TASAF Wawe Wamelipwa Fedha Zao” – Mh. Simbachawene.
Kauli hii imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Geroge Simbachwene alipokuwa ziarani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kukagua miradi inayotekelezwa na wanufaika wa Kaya Masikini TASAF, Februari 22, 2024.
Mheshimiwa Simbachawene amemuagiza Meneja wa Miradi Ndugu Paul Kijazi, ambaye anasimamia miradi yote inayotekelezwa na wanufaika wa Kaya Masikini ambao wapo kwenye mpango wa TASAF.
“Isizidi mwezi Machi walengwa wote wawe wamelipwa fedha zao ambazo wamezifanyia kazi kwa kubuni na kutekeleza miradi hii. Tena nimefurahishwa na utekelezaji wa miti ya matunda kwenye Taasisi kama shule. Hii itasaidia watoto kupata lishe, na kujifunza elimu ya kujitegemea. Kuanzia sasa miradi yote itekelezwe kwenye maeneo ya Taasisi ili miradi hiyo iwe endelevu”.
Mheshimiwa Simbachawene ameweza kukagua miradi ambayo imebuniwa na walengwa wa TASAF katika Kata ya Kising’a Kijiji cha Kinywang’anga ambapo kuna mradi wa birika la kunyweshea mifugo, na Kata ya Migoli ambapo kuna shamba la miti ya mtunda mbalimbali katika Shule ya Msingi Migoli.
Aidha ameendelea kusema, “kwa wale ambao wameshapata unafuu wa maisha basi wanaweza kujiondoa na kuwapisha wengine ili nao wanufaike na kujikwamua katika mpango huu. Mpango huu husaidia sana wenye ulemavu katika kaya masikini hivyo wapewe kipaumbele”.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Stephen Mhapa amepata nafasi ya kuwasilisha ombi la kibali cha Ajira kwa Watendaji wa Vijiji, kwani Halmashauri inakabiliwa na uhaba mkubwa wa Watendaji, zaidi wa Vijiji 30 havina Watendaji.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa