Maofisa kutoka Kituo cha Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public Private Partinership Center - PPPC), wametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa ajili ya kupitia maeneo ya uwekezaji, kuvutia Wawekezaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Maafisa hao ni Dr. Moshi Derefa na Bi. Ziada Saburi wamefanya ziara hiyo Aprili 04 - 05, 2025 kwa kuongozwa na Maafisa wa Uwekezaji kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Awali Maafisa hao walitoa mafunzo ya dhana ya PPPC kwa Maafisa Biashara na Uwekezaji, na kusema kuwa, Taasisi inatakiwa kuibua miradi yenye sifa kwa utaratibu wa PPP, kuandaa maandiko ya miradi itakayopendekezwa, kuandaa matangazo ya miradi kwa ajili ya kupata wawekezaji, na kuweka miradi kwenye ramani ya Halmashauri.
Maeneo waliyotembelea ni pamoja na Kata ya Migoli Kijiji cha Migoli kwenye Soko la Samaki kuwekeza Kiwanda cha Kuchakata Minofu ya Samaki. Eneo lipo pembezoni mwa Bwawa la Mtera. Kata ya Nduli kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli ya Kitalii, eneo lipo pembezoni mwa barabara ya Iringa - Dodoma, Kata Kising'a Kijiji cha Igingilanyi eneo la mapumziko, burudani na michezo mbalimbalu, pia eneo la ujenzi wa kituo cha mafuta. Kata ya Kitanzini ujenzi wa Hosteli na Kata ya Makorongoni ujenzi wa Hoteli (Lodge) na vyumba vya maduka, Kata ya Gangilonga eneo la Posta ujenzi wa nyumba yenye vyumba vya ofisi, eneo karibu na Siasa ni Kilimo ujenzi wa kumbi za mikutano.
Kata ya Nyang'oro kwenye msitu wa asili kwa ajili ya kuhifadhi hewa ukaa, Kata ya Itunundu Kijiji cha Igodikafu ujenzi wa kiwanda cha kukoboa na kupaki mchele pia kilimo cha miwa. Kata ya Idodi kijiji cha Tungamalenga kilomita 10 kufikia lango la kuingia Hifadhi ya Ruaha, ujenzi wa Hoteli ya Kitalii, Kata ya Ulanda Kijiji cha Kikongoma chenye historia muhimu ya Chifu Mkwawa na Mama yake, chemchem ya maji ya moto, ujenzi wa Hoteli ya Kitalii na Kata ya Kalenga Kijiji cha Kalenga ujenzi wa Shule ya Msingi yenye Mtaala wa Kiingereza, eneo lipo pembezoni mwa barabara ya kwenda Mbuga ya Ruaha.
"Tumia Fursa, Karibu Uwekeze Halmashauri ya Wilaya ya Iringa"
@ortamisemi
@wizaraadedha
@pppenter
@rsiringa
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa