Hatimaye Barabara ya Ipogolo – Kilolo Yapata Mkandarasi wa Uhakika
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. Innocent Bashngwa (MB), Oktoba 05, 2023 ameshuhudia zoezo la utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara yenye urefu w Km 33.61 kwa kiwango cha lami, ambayo inatoka Iringa Ipogolo kwenda Wilaya ya Kilolo itakayogharimu zaidi ya Tsh. Bilioni 60.144.
Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini Mhe. Bashungwa amesema kuwa, Wilaya ya Kilolo ni Wilaya iliyojikita katika uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula, hivyo barabara hiyo italeta mageuzi makubwa katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Kilimo ambapo wakulim na wafanyabisahra watasafirisha bidhaa salama na kwa wakati. Pia utavutia wawekezaji kuwekeza Wilayani humo.
Aidha Mh. Bashungwa amesema, suala la barabara hiyo imekuwa ni kilio cha muda mrefu sana kwa wananchi wa eneo hilo, hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshapata mwarobaini wa kilio hicho. Sasa wana Kilolo wazidi kufanya kazi mambo mazuri yanakuja.
Akitoa taarifa ya Mkoa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Omary Dendego ametoa shkurani kwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi mingi ya maendeleo, ambapo kupitia miradi hiyo wananchi wengi wamepata ajira.
Mradi huu ni moja ya miradi ambayo inatekelezwa na Serikali ikishirikiana na Benki ya Dunia kupitia Program ya Roads to Inclusion and Social Economic Opportunities (RISE), ambapo kukamilika kwa barabara hii utaleta ufanisi mkubwa katika Sekta ya Usafirishaji.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa Iringa (Tanroads) Ndugu Mohamed Besta ameahidi kusimamia vizuri ujenzi wa barabara hiyo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa