Shirika la Helen Keller Internation kupitia Wataalamu wa matibabu ya macho kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na Mkoani wameleta tabasamu kwa wananchi wa Pawaga na maeneo mengine ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kutoa matibabu ya vikope.
Akizungumza wakati wa zoezi la kuwatembelea wagojwa waliopata huduma ya matibabu (monitoring visit) lililofanyika kwenye Kata ya Ilolompya Mei 30, 2024 Dr. Roida Mkalimoto amesema lengo ni kuona maendeleo ya watu waliokwisha kupata huduma ya matibabu ili kubaini ikiwa kuna changamoto ya kufanyia kazi.
Kwa upande wao, wananchi wa maeneo mbalimbali kata ya Ilolompya, wamepokea kwa furaha huduma hiyo na kusema kuwa imewasaidia sana na kuwawezesha kuendelea na shughuli zao za kila siku bila usumbufu. Aidha wameishukuru Serikali na wadau kutoka Shirika la Helen Keller Internation kwa kufanikisha zoezi hilo.
“Mimi mara ya kwanza wakati huduma haijanifikia nilikuwa haya macho sioni, machozi yalikuwa yananitoka nikiangalia naona kama kuna moshi lakini wataalamu waliponifikia na kunitengeneza haya macho mpaka sasa naona vizuri na shughuli zangu zakilimo nimelima kama kawaida na kazi za nyumbani naendelea kufanya” Amesema Helena Mgimwa.
Shirika la Helen Keller Internation ni shirika la Kimarekani lisilo la faida ambalo linapambana na sababu na matokeo ya upofu na utapiamlo kwa kuanzisha program zinazozingatia usahihi na utafiti wa maono, afya na lishe.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa