Ibo Italia ni Shirika la Kiitalia ambalo ni Mdau mkubwa sana kwa Mkoa wa Iringa katika kusaidia mambo mbalimbali.
Mei 17, 20204 Shirika hilo limekabidhi majengo ya vyoo vyenye matundu 16 vya wanafunzi, (Wasichana matundu 8 na Wavulana matundu 8), Shule ya Msingi Kidamali Kata ya Nzihi, ambapo mradi huo umetekelezwa kwa kushirikiana na mashirika ya Call Africa, na COPE ambayo yenye Makao Makuu yake nchini Italia.
Akitoa taarifa ya mradi huo Afisa Mradi Ndugu Elikana Katambi amesema kuwa, mradi umetumia kiasi cha Shilingi Milioni 82.62 na sasa mradi umekamilika kwa 100%.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mwal. David Mlowe amesema, anawashukuru Ibo Italia kwa kujitolea kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo kutoa gari aina ya Hice kwa ajili ya wanafunzi wa Mahitaji Maalum wa Shule ya Kipera.
Ameongeza kusema kuwa, gharama zilizotumika katika mradi ni kubwa sana, hivyo amewaomba wananchi na wanafunzi kuutunza mradi huo kwa kufanya usafi. Pia kuweka mpango wa kimkakati kwa kuchangia ili kuendeleza mradi huo kwa ajili ya malipo ya umeme na maji,
Aidha, Ndugu Mloewe amesema kuazisha Clabu ya SWASH ambayo itakuwa Balozi katika kusimamia suala zima la usafi na kuripoti uharibufu ambao utaweza kutokea katika mradi huo wakati ukiendelea kutumika.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidamali amesema, kushukuru ndiyo kuomba tena, hivyo ameomba Shirika kujengewa vyoo vya Walimu, kwani kwa sasa Walimu hawana sehemu maalum ya kujisitiri.
Kadhalika Mhandisi wa vyoo hivyo ameomba uongozi wa Shule na Kijiji kuondoa/kukata miti ambayo ipo jirani na mradi huo ili isilete uharibifu kama kudondokea katika majengo hayo au kupukutisha majani na kuchafua mazingira
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa