Vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wadogo vyajitokeza na kutoa salamu za shukrani kwa Serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshwaji
Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2025, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Imefanya maadhimisho hayo ngazi ya Wilaya Machi 07, 2025 yaliyoambatana na shughuli mbalimbali. Maadhimisho yamefanyika katika viwanja vya Makao makuu ya Halmashauri – Ihemi yaliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James.
Aidha Mhe. Kheri James amekagua Maonesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiriamali wadogo ambao ni wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 ya wanawake, vijana na watu wenye Ulemavu inayotolewa na Halmashauri ya Wilaya sanjari na vikundi vinavyosimamiwa na wadau kutoka asasi zisizo za kiserikali.
Sherehe hizi zimepambwa na kaulimbiu isemayo; “Wanawake na Wasichana 2025; Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji” ambazo zimeambatana na kufanya matendo ya huruma ambapo Watoto wenye uhitaji kwa mahitaji mbalimbali walipatiwa misaada hasa kwenye mahitaji ya kibinadamu.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa