IRINGA DC YAJIWEKA TAYARI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2024
Mratibu wa Mbio za Mwenge Mkoa Wa Iringa ndg. Steven Sanga ameipongeza kamati ya Mbio za Mwenge Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa maandalizi ya Jumla ya Kupokea Mwenge wa Uhuru 2024 kwa kukamilisha Miradi itayo kaguliwa na Mwenge wa Uhuru
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo Ndg. Steve Sanga Amesisitiza kurekebisha baadhi ya Maeneo na taarifa za miradi hiyo ili ziweze kuendana na hadhi ya Mwenge wa Uhuru 2024.
Miradi itakayo kaguliwa na kuzinduliwa na Mwenge Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ni hifadhi ya mazingira katika chanzo cha Maji Kilichopo Kijiji Cha Muwibi, Miradi ya Elimu (vyumba Vya Madarasa, Mabweni), mradi wa kilimo na usindikaji mazao ya kilimo Kidamali (Shafa Agro), klabu za kupambana na rushwa, madawa ya kulevya, na lishe, mradi wa Barabara, afya na maji .
Nae Bi. Sakina Mgaya ambaye ni Mratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Amesema amepokea marekebisho yote yaliyotolewa na Kamati ya Mwenge Mkoa Ili kufanikisha miradi kuwa ma tija kwa Jamii na kusisitiza kwa watendaji, walimu, wenyekiti kuhimiza Wananchi Kujitokeza wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024.
Mwenge wa Uhuru 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa unatarajiwa kupokelewa mnamo mwezi June, 2024 ukitokea katika Halmashauri ya Manispaa Iringa na baadaye kukabidhiwa Mkoani Dodoma ambapo kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka 2024 " Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa TAIFA Endelevu"
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa