Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi. Doris Kalasa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kupata Hati safi. Bi. Kalasa ameyasema hayo wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani uliofanyika tarehe 14.06.2024 katika ukumbi wa makao makuu ya Halmashauri – Ihemi.
“Nichukue fursa hii pia kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kupata Hati safi ya Ukaguzi kwa mwaka ulioishia mwezi tarehe 30 Juni 2023, hongereni sana. Matokeo haya ni ishara ya ushirikiano uliopo kati ya Mhe. Mkuu wa Wilaya, kamati ya usalama ya Wilaya, waheshimiwa wabunge, waheshimiwa madiwani na watendaji wa Halmashauri chini ya usimamizi wa chama cha mapinduzi”, amesema Bi. Diris Kalasa.
Aidha, Bi. Kalasa ameitaka Halmashauri kuhakikisha kuwa hoja zote zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka 2022/2023, hoja za miaka ya nyuma na maagizo ya kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali zinafanyiwa kazi ipasavyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe. Steven Mhapa amemhakikishia Katibu Tawala Iringa kuwa maagizo yote yaliyotolewa yamechukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa kazi na kuwakumbusha watendaji kuwa kila mmoja awajibike kwa nafasi yake kwani hakuna hoja inayojizaa yenyewe bali hoja zimezalishwa na watu.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa