Mratibu wa mbio za Mwenge Mkoa wa Iringa ndg. Atilio Mganwo amaeipongeza kamati ya Maandalizi ya Mapokezi ya Mbio za Mwenge ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kufanya maandalizi na kukamilisha Miradi mingi ambayo itazinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2024.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo Ndg. Mganwo Amesisitiza kukamilishwa kwa baadhi ya marekebisho ambayo yametolewa na Kamati ya mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Iringa 2024. Huku akisitiza Miradi hiyo kuendana na kauli mbiu ya mwaka huu.
Baadhi ya Miradi iliyokaguliwa ni Chanzo Cha Maji kilichopo Kijiji Cha Muwibi. (Chodota), vyumba vya madarasa na mabweni ya wanafunzi, Barabara, na vituo vya kutolea huduma ya Afya, ambavyo vinatarajiwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2024.
Naye Bi. Sakina Mgaya ambaye ni Mratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Wilaya ya Iringa amesema atafanyia kazi kwa haraka marebisho yaliyo tolewa na Kamati ya Mwenge Mkoa Ili kufanikisha Miradi iyo kuwa na tija kwa jamii na kusisitiza wananchi, watendaji pamoja wenyekiti kujitokeza wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru.
Mwenge wa Uhuru 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa unatarajiwa kupokelewa mnamo mwezi June, 2024 ukitokea katika Halmashauri ya Mji Mafinga na baadaye kukabidhiwa Mkoani Dodoma ambapo kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 ni, "Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa TAIFA Endelevu".
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa