JAMII YAASWA KUTUZA MIUNDOMBINU YA AFYA IRINGA DC
Haya yamesemwa na Peres Boniphace Magiri Mkuu wa Wilaya ya Kilolo alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego 24.12.2023 katika kijiji cha Matembo ambapo kuna Zahanati iliyojengwa kwa Ufadhili wa Kampuni ya ASAS kuanzia mwanzo hadi kukamilika kwake.
”Tunatakiwa kuilinda na kuitunza miundombinu ya afya, hakuna sababu ndani ya mwaka mmoja tuanze kuhitaji ukarabati hilo naamini mtazingatia si hapa tu bali ni maeneo yote ambapo tuna miundombinu hii ambayo tunasema imezinduliwa katika vituo vingine vinane katika Wilaya yetu ya Iringa. “ amesema Mhe. Magiri.
Vituo vya kutolea huduma ya afya vilivyozinduliwa ni 8 ambavyo ni;
Pia kumefanyika upanuzi wa vituo viwili vya afya ambavyo ni Isimani na Malengamakali kwenye eneo la majengo ya upauaji, Maabara, OPD, Mochwari, nyumba za watumishi na majengo ya huduma ya uzazi afya na mtoto.
Zoezi hili la uzinduzi wa vituo vya kutolea huduma za afya limeenda sambamba na uzinduzi wa maboresho ya huduma kwenye Hosptali ya Wilaya ya Iringa (Igodikafu). Maeneo yaliyoboreshwa ni kwenye upande wa huduma ya upasuaji kwa akimama wajawazito huduma ambayo mwanzoni haikuwepo, huduma za meno, huduma za macho na x-ray.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni ya ASAS ameahidi kujenga zahanati nyingine moja na kusaidia maboresho ya zahanati ya Kising’a ili iwe kituo cha Afya.
Naye Diwani wa Kata ya Kising’a Mhe. Ritha Mlagala ameishukuru Serikali chini ya Rais wa awamu ya sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutengeneza mazingira mazuri ya wadau kuweza kushirikiana na jamii kufanya shughuli za maendeleo. vilevile ameishukuru kampuni ya ASAS kwa kuwajengea Zahanati na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa Kutoa milioni 14 kwa ajili ya vifaa tiba.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa