Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe. Stephen Mhapa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa ameikumbusha jamii kuchukua hatua dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI kwani UKIMWI unapunguza nguvukazi ya Taifa na kuzalisha utegemezi kwa watoto kukosa malezi ya wazazi. Mhe. Mhapa mezungumza hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Isimani Tarafani Kiwilaya 01.12.2023.
“Serikali yetu ya Rais Samia Suluhu Hassan inaleta fedha nyingi sana kwenye sekta mbalimbali kujenga miundombinu lakini kama hatutachukua tahadhari dhidi ya VVU/UKIMWI, hivyo vitu vinavyofanywa tutaishia kuvisikia tu na vitakosa wa kuvitumia,” amesema.
Eidha Mhe. Mhapa ameiasa jamii kutoa matunzo na malezi kwa watoto ili waweze kufikia ndoto zao. “Hawa watoto wote wanaosoma wakikosa malezi ya Wazazi na familia maana yake ndoto zao zinapungua kwa sababu hawana wa kuwatunza, leo hii tunapata elimu bila malipo lakini ukweli ni kwamba bado yanahitajika matunzo na huduma mbalimbali mzazi inabidi apambane nazo kwaajili ya mtoto wake” amesema.
Kwa upande wake mmoja wa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU/UKIMWI Bi Rehema Michael Sanga ametoa wito kwa jamii kujitokeza na kujua afya zao na kwa wale watakaopatikana na maambukizi wasiache kufuatilia afya zao na kuwa na ufuasi wa dawa bila kuacha kwani hata yeye ana miaka mingi akiwa na maambukizi lakini kwa kujiweka wazi ameweza kufanya ufuasi bora wa dawa na hatimaye afya yake ni nzuri na ameweza kulea familia yake.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Saumu Kweka amewashukuru wananchi wote wa kijiji cha Kihorogota kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki maadhimisho haya sanjari na wadau mbalimbali walioshiriki moja kwa moja kufanikisha shughuli hii wakiwemo wadau kutoka Shirika la Compassion
Maadhimisho haya yamefanyika yakiwa na kauli mbiu isemayo, “Jamii Iongoze Kutokomeza UKIMWI”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa