KAKAKUONA KAONEKANA KIJIJI CHA IHEMI
Mkurugenzi Mtendaji(W) akiongozana Wataalamu wa wanyamapori kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa leo tar 14.07.2023 wamefika katika kijiji cha Ihemi ili kushuhudia uwepo wa mnyama aina ya Kakakuona aliyeonekana kwenye kijiji hicho na kuhakikisha kuwa anapelekwa sehemu salama anakotakiwa kuwa.
Akiongea na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ihemi pamoja na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja amewashukuru wananchi kwa kutoa taarifa kwa wakati na kuwaasa kuwa utoaji huu wa taarifa uwe endelevu pale linapotokea jambo kama ambavyo walikuwa wakitoa taarifa kuhusu suala la simba hapo nyuma.
Wakili Mhoja amesema jamii inaamini kuwa uwepo wa kakakuona huambatana na Baraka, wakati mwingine mnyama huyo huwekewa vitu vizuri na kuviendea kuashiria hali njema au tahadhari na huenda ikahusishwa na Neema wakati ambapo Halmashauri inajiandaa kuhamia kwenye jengo Jipya lililopo kwenye Kijiji hicho cha Ihemi.
Naye afisa Wanyamapori ndugu Charles Mdendemi amesema, wanamchukua mnyama huyo na kumpeleka kwenye hifadhi ya pori la Mbomipa sehemu ambayo ina mazingira mazuri na yenye kufaa kwa mnyama huyo.
Kakakuona ni wanyama ambaye amepambika/kufunikwa na magamba na wana mkia mrefu. Chakula cha mnyama huyu ni mchwa, sisimizi na wadudu wengine ambao huwakamata kwa ulimi wao mrefu wenye kunata.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa