Kamati ya Elimu Afya na Maji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ikiongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Benito Kayugwa imefanya ziara ya kutembelea kituo cha kufua umeme kilichopo Mtera kujionea shughuli zinazofanyika huko.
Ziara imefanyika Mei 27, 2024 ambapo wajumbe wamepata fursa ya kupokea taarifa ya namna kituo kinavyoendeshwa changamoto mbalimbali na kisha kutembelea mitambo ya uzalishaji na kujionea jinsi inavyofanya kazi kufua umeme.
Mwenyekiti wa kamati Mhe. Benito Kayugwa ametoa shukrani kwa uongozi wa kituo kufuatia mapokezi ya ziara yao na kuahidi kutoa ushirikiano na kuwa mabalozi wazuri wa kituo cha Mtera kwa elimu waliyoipata.
Naye Meneja wa kituo Eng. Edmund Seif amedokeza mchakato wa kufikisha umeme kwenye vijiji na maeneo ya jirani kutokea kwenye kituo cha Mtera ambapo wanashirikiana na REA kufanikisha zoezi hilo. Sanjari na hayo, Eng. Edmund amesema yupo tayari kushirikiana na viongozi wa kijamii na kwamba kama kuna jambo lolote wanaweza kushirikishwa ili jamii inayozunguka iwe na ustawi mzuri.
Kituo cha kufua umeme cha Mtera kinazalisha megawati 80 ambazo huunganishwa kwenye gridi ya Taifa.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa