Kamati Ya Fedha Utawala Na Mipango imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ambayo inaendelea kutekelezwa katika Halmashauri Julai 20, 2023 ambapo ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Ponziano Kayage Diwani wa Kata ya Kihorogota
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni;-
Kamati imepongeza kazi kubwa na nzuri inayofanyika na inayoendelea kufanyika. Pia Mhe Kayage ametoa pongezi kwa viongozi walioshiriki kwenye usimamizi wa kazi hizo akiwemo Mtendaji wa Kata ya Magulwa Bi. Neema Kameka na Mtendaji wa Kijiji cha Ihemi Bi Happiness Mkongwa kwa kujitoa kwao.
Aidha kwenye ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ihemi Mhe kayage amesema kuwa kwa hatua iliyofikiwa kwa michango ya wananchi nawadau ni kubwa hivyo wamalizia makuta kisha Halmashauri ifanye jitihada za kuwaunga mkono ili kumalizia kazi.
Kwa upande wa Shamba la Parachichi wajumbe wameshauri kuwa, wataalamu wa kilimo watoe ushauri unaofaa ili mradi huo uwe na tija kwa Halmashauri.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa