Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mheshimiwa Stephen Mhapa, imefanya ziara kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri Februari 14, 2024.
Ziara hiyo ilianzia katika shule ya Msingi Lyamgungwe iliyopo Kata ya Lyamgungwe, kuna ujenzi wa vyoo matundu 19. (Wasichana matundu 10, Wavulana matundu 6 na Walimu matundu 3), mnara wa kuweka tanki la maji na kichomea taka.
Kiasi cha Shilingi Milioni 50 zilitolewa na Serikali katika mradi huo na nguvu za wananchi wamechangia kiasi cha Shilingi Milioni 11.3 na kufanya jumla ya kiasi cha Shilingi 61.8 hadi kukamilika kwake. Mradi ulianza mwaka wa Fedha 2022/2023 umekamilika kwa 100% na unatumika.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Lyamgungwe ameomba kuwa, kama ikitokea ukaletwa mradi mwingine wanaomba kupewa usafiri kwa ajili ya kusafirishia madini ujenzi, pia huduma ya maji ya kudumu iwepo ili kurahisisha utendaji kazi.
Kamati imepongeza mradi kwenda vizuri na kuomba mradi utunzwe vizuri kwa usalama wa afya zao.
Kamati pia imetembelea Kijiji cha Ibumila ambapo kuna shamba la parachichi na kujionea shughuli zilizofanyika hapo.
Akitoa lengo la mradi wa shamba hilo Bi. Luvy Nyallu amesema ni kuweka shamba darasa, kuongeza kipato baada ya mavuno. Shamba hilo lenye ukubwa wa heka 12 ambapo imepandwa miche 912 na imetumia kiasi cha Shilingi Milioni 30 na kwamba msimu wa tano wanategemea kuvuna kukadiria kupata zaidi ya Shilingi Milioni 47.
Kamati imeridhia mradi huo na kutoa ushauri kuwa, ujengwe uzio ili kuimarisha ulinzi.
Wakisalia hapo Ibumila katika mabwawa ya samaki manne ambayo yamejengwa kwa lengo la kufanya shamba darasa na kuongeza kipato. Kiasi cha Shilingi Milioni 116.3 zilitengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Vifaranga zaidi ya 9,600 vitapandwa na kilo zaidi ya 12,800 zitapatikana katika mabwawa hayo. Hatua ya mradi ni 100%.
Kamati imeridhishwa na mradi huo na kutoa ushauri kuwa, zipandwe nyasi kando ya mabwawa ili kuzuia mmomonyoko wa udongo.
Kamati pia imepata nafasi ya kutembelea Shule ya Sekondari Lumuli iliyopo Kata ya Lumuli katika ujenzi wa vyoo vya wanafunzi matundu 9. Kiasi cha Shilingi Milioni 7.8 kilitengwa na nguvu za wananchi ni Shilingi Milioni 6 na kufanya jumla ya fedha kuwa Shilingi Milioni 13.
Kamati imeridhia mradi na kutoa ushauri kuwa, ujenzi ukikamilika vyoo visitumike hadi mfumo wa maji utakapokuwa tayari. Ujenzi umefikia 90% ujenzi unaendelea.
Kamati imefika Shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda na kujionea mradi wa ujenzi wa Bweni la Wasichana lenye uwezo wa kulawa wanafunzi 80, ambapo kiasi cha Shilingi Milioni 130 zililetwa kutekelezwa mradi.
Mradi ulianza Oktoba 2023 na ulitakiwa kukamilika Januari 2024, Lakini kutokana na changamoto mbalimbali hadi sasa ujenzi unaendelea na sasa umefikia 90%.
Kamati imeridhia mradi na kushauri kuwa, Mkandarasi aongeze kasi ya ujenzi, na ametakiwa hadi kufikia Febaruari 20, awe amekamilisha mradi na kukabidhi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa