Yakagua miradi minne inayotekelezwa yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.8
Kamati Ya Fedha, Utawala Na Mipango yafanya ziara kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mapema Januari 30, 2025.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni; ujenzi wa nyumba za walimu (2 in 1) na mabweni 2 shule ya sekondari Weru kwa jumla ya Sh. 360,000,0000, ujenzi wa kituo cha Afya Mahuninga sh. 666,427,801/-, ujenzi wa mabweni 2 shule ya sekondari Makifu sh. 260,000,000/- na ujenzi wa shule mpya ya sekondari Mapogoro sh. 583,180,028.
Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe. Kindole amepongeza kazi inayoendelea na usimamizi wake na kutoa wito wa kuongeza kasi ya ujenzi ili kuendana na muda uliopangwa kwa mjibu wa mikataba.
Miradi yote hii ipo katika hutua mbalimbali za utekelezaji ambapo shule ya sekondari William Lukuvi ya Kijiji cha Mapogoro imeshaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2025.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa