Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Yafanya Ziara Kukagua Miradi ya Maendeleo kwa Robo ya Tatu 20222/2023
Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango imefanya ziara kukagua miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa katika Halmashauri kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.
Kamati hiyo ambayo imeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Methew Nganyagwa, imeanza kwa kwenda katika Kijiji cha Ilambilole Kata ya Kising’a kukagua mradi wa kinga maji ambao unatekelezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kupewa ajira ya muda. Kamati baada ya kuona mradi wameshauri mambo mbalimbali ikiwemo kumalizia mradi kwa wakati. Mradi umepewa siku 60 hadi ukamilike na ulianza 01/03/2023.
Pia Kamati imeweza kwenda hadi kijiji cha Makuka Kata ya Izazi katika mradi wa ujenzi wa Josho, ambapo mradi huu unatekelezwa na Halmashauri kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kupitia mpango wa Sustainable Landscape Restoration – SLR. Mradi ulianza Machi, 2023 na unatarajiwa kukamilika Juni 15, 2023. Kamati imeshauri kuharakisha mradi huo ili ifikapo Juni 15, 2023 uwe umekabidhiwa.
Kamati imeendelea kufanya ziara yake hadi Kijiji cha Mnadani Kata ya Izazi ambapo kuna mradi wa ufugaji ng’ombe 3 wa maziwa, ambao unafanywa na kikundi cha Tumsifu chenye watu 6 wenye Ulemavu, ambapo kuna wanaume 4 na wanawake 2. Ng’ombe hawa wametolewa kwa Ruzuku kutoka Ofisi a Makamu wa Rais Mazingira kwa mpango wa Sustainable Landscape Restoration – SLR.
Aidha Kamati imetembelea katika Kijiji cha Migoli Kata ya Migoli katika mradi wa upandaji miti ya matunda. Mradi huu unatekelezwa na Walengwa wa TASAF kwa kupewa ajira ya muda. Miti iliyopandwa ni aina ya miembe, machungwa, malimao na mapera.
Kamati haikuishia hapo, bali imeenda kijiji cha Mbweleli Kata hiyo ya Migoli katika mradi wa utengenezaji barabara inayolimwa kwa njia ya mikono, ambapo mradi unatekelezwa na Walengwa wa TASAF kwa kupewa ajira ya muda.
Vilevile katika Kata hiyo ya Migoli Kijiji cha Makatapola kuna mradi wa ufugaji mbuzi, ambapo unatekelezwa na kikundi cha Nanyolai chenye watu 20 wakiwa wanawake 17 na wanaume 3. Kikundi hiki kilipatiwa Fedha ya Ruzuku zaidi ya Milioni 10 na kuanzisha mradi wa mbuzi 95. Hadi sasa mbuzi 37 wamezaa na kupatikana ndama 39 na kufanya jumla ya mbuzi kuwa 134. Mradi ulianza mwezi Machi, 2023.
Kwa niaba ya Kamati Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Methew Nganyagwa, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi ili kutekeleza miradi mbalimbali katika Halmashauri. Mheshimiwa Nganyagwa amewasihi wote wanatekeleza miradi hiyo kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi ili ikitokea fursa nyingine wasiweze kukosa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja, ametoa rai kwa kikundi cha Ufugaji mbuzi cha Nanyolai kuendelea kupanda miti ili kuhifadhi mazingira na kuwa chanzo cha mvua. Kutokana na Tabia Nchi mazingira yanapoeza uoto wa asili na kusababisha jangwa kubwa.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa