Kamati ya Fedha na Mipango Yafanya Ziara Kukagua Miradi ya Maendeleo
Kamati ya Fedha na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imefanya ziara kukagua miradi ya maendeleo Septemba 24, 2024, na kuona nini kimefanyika katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Kamati hiyo imetembelea baadhi ya miradi na haijaridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuchelewa kukamilika kwake.
Akijibu maswali yaliyoulizwa na Kamati hiyo, Mhadisi wa Wilaya Ndugu Nicco Kasililika amesema, “miradi hiyo imechelewa kutokana na ufinyu wa fedha ambazo zimetolewa na Serikali ikilinganishwa na ukubwa wa miradi, hivyo kupelekea kuomba kuongezewa fedha ili kukamilisha miradi hiyo”.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndugu Robert Masunya akitoa majibu ya nyongeza amesema, “tunajitahidi kuomba fedha hizo hizo ili ujenzi uendelee kwani ulisimama kutokana na sababu hizo zilitajwa na Mhandisi, pia kusimama kwa mifumo ya fedha mara nyingi pia sababu”.
Ndugu Masunya ameongeza kusema kuwa, pamoja na mapungufu hayo atajitahidi kuyafanyia kazi na kukamilisha majengo hayo.
Baadhi ya miradi iliyokaguliwa na Kamati hiyo ni ujenzi wa nyumba ya Mkurugezi, nyumba tatu za Wakuu wa Idara, Uzio wa jengo la Halmashauri na nyumba ya mlinzi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa