Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria Yafurahishwa na Mradi wa Shamba la Parachichi
Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala, Sheria na Katiba linayoongozwa na Mheshimiwa Joseph Kizito Mhagama imetembelea na kukagua mradi wa shamba la matunda ya parachichi ambao umebuniwa na wanufaika wa mfuko wa kusaidia Kaya Masikini – TASAF, Machi 12, 2024.
Mradi huo ambao upo katika Shule ya Msingi Ibumila Kata ya Mgama, na kwamba walengwa hao walipomaliza kulima waliweza kukabidhi shamba hilo katka Taasisi hiyo ya shule ili waweze kunufaika wanafunzi wa shule hiyo.
Mheshimiwa Mhagama amewapongeza sana walengwa hao kwa kubuni mradi huo na kuuweka katika Taasisi ya Shule, ambapo itakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi kwa kupata lishe na kupunguza udumavu.
Kamati hiyo ambayo ilikuwa na mwenyeji wa Wizara yenye dhamana ya Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo Naibu Waziri wake Mheshimiwa Ridhiwan Jakaya Kikwete aliongoza Kamati hiyo kukagua shamba hilo.
Naye Diwani wa Kata ya Mgama Mheshimiwa Job Mbwilo aliweza kuwasilisha ombi la kujengewa madarasa katika shule hiyo, ambapo yaliyopo yamechakaa. Ombi lilisikilizwa na Mheshimiwa Kikwete ameahidi kujenga madarasa mawili.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa