Kamati ya Lishe Yakutana Kujadili Afua za Lishe
Katika mapambano dhidi ya udumuvu, Kamati ya Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, imekutana mapema leo Novemba 15, 2023 kwa ajili ya kupeana mikakati ya jinsi ya kuongeza mapambano hayo ya udumuvu.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Afua za Lishe kwa Robo ya Kwanza (Julai – Septemba), Afisa Lishe Wilaya Bi. Tiliza Mbulla amesema, “Halmashauri imeendelea kupambana na matatazo ya lishe duni kwa makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanaokadiriwa kuwa 43,711, kina mama wajawazito wanaokadiriwa kuwa 12,614 kwa mwaka na pia hali ya lishe ya makundi mengine ya wananchi wanaokadiriwa kuwa 315,354 kwa ujumla wao”.
Bi. Tiliza ameendelea kusema, “shughuli za mapambo dhidi ya lishe duni zinafanyika kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa lishe kwa kuzingatia mikakati ya lishe na kufuata vipaumbele vilivyowekwa katika Mpango Jumuishi wa Taifa wa Lishe (NMNAP II 2021/22 – 2025/26)”.
Bi. Tiliza amefafanua kuwa, utekelezaji huu umekuwa na ufanisi kwa uratibu wa watoa huduma 268 wa ngazi ya jamii (CHWs) pamoja na watoa huduma wa afya katika vituo 101 vya kutolea huduma za afya, kwani wamejengewa uwezo katika masuala ya lishe, lengo ikiwa ni kupambana na udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano, pia kutoa elimu kwa vijana balehe na wanawake walio katika umri wa kuzaa.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa