Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Iringa yamuelewa Rais Samia.
Na Maafisa Habari (Iringa -DC)
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi jana imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa na serikali ya awamu ya sita huku wakimpongeza Mh.Rais kwa jitihada zake za kuboresha Sekta za Afya na Elimu.
Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mh.Costantino Kihwele amesema pamoja na miradi hiyo mizuri na kukamilika kwa wakati ni jukumu la kila mmoja kuitunza lakini kubwa Zaidi wanafunzi ambao ni walengwa kuhakikisha wanayatumia madarasa hayo.
“Mh.Rais atafarijika akisikia madarasa aliyoyaleta katika maeneo yetu yanatumiwa na watoto, ambao wamefaulu na kuchaluliwa kujiunga na darasa la kwanza kwa shule shikizi na kidato cha kwanza kwa shule za sekondari”alisema.
Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mh.Gama J.Gama amewataka viongozi wa Chama hiko katika kazi za kata na vijiji kuendelea kuwahimiza wananchi kuibua miradi katika maeneo yao ili serikali yao iweze kuona na kuwashika mkono.
“Ndugu zangu siku zote ili uweze kupata fedha za serikali kwa haraka ni lazima kuwepo na jitihada za maendeleo ambazo ninyi wananchi mmeanzisha na serikali yenu sikivu ya Chama Cha Mapinduzi itawaletea fedha za kumalizia miradi mlioanzisha”alisema na kuongeza;
“Waambieni wananchi kuwa sasa hivi miradi inayoendelea katika maeneo yao wanapaswa kushiriki na kujitolea miradi ambayo ilikatazwa kuchangia ni miradi ya UVIKO-19 amabyo imeshakamilika na itaanza kutumiwa tarehe 17 mwezi huu wa Januari”alisema.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa