Makinda atoa neno kwa Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini kuhusu Sensa 2022
Na Zaituni Gwaja
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Kamisaa wa Sensa Bi. Anna Makinda amezungumza na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali katika kikao kinachoendelea kufanyika Jijini Tanga katika Ukumbi wa Regal Naivela juu ya majukumu yao katika suala zima la Sensa.
Ambapo Kauli Mbiu ya Mkutano huo ni “Mawasiliano ya Kimkakati Nyenzo Muhimu Kufanikisha Sensa ya Watu na Makazi 2022”
Bi. Makinda amesema kuwa, sensa ni jambo la lazima katika kila Taifa, Kwa Taifa letu sensa hufanyika kila baada ya miaka kumi na kwa Tanzania ni sensa ya sita tangu kuungana kwa Tanganyika na Zanzibar, na mwaka huu Sensa itafanyika mwezi Agosti, 23.
“Itakuwa sensa ya kidigitali kwani itatumia sana mifumo (TEHAMA), ambayo itahesabu hadi majengo, ili kujua kuna majengo mangapi ya Serikali, Taasisi, makazi n.k.” amesema.
Bi Makinda ameendelea kusema kuwa, zitatumika rasilimali zilizopo ili kufanikisha zoezi hili, kwani hakuna bajeti iliyoandaliwa kwa kazi hii.
Ameongeza kusema kuwa, sensa hii ni shirikishi na Maafisa Habari ndiyo hasa wanatakiwa kuifanya kazi hii kwa kutangaza na kutoa takwimu sahihi. Sensa hii watakaonufaika ni vijana kwani asilimia kubwa huwa wanatumia mitandao ya kijamii, pia itasaidia kujua vijana wangapi wameajiriwa, hawana ajira, na wangapi wamejiajiri.
Katika maandazili haya ya Sensa ni 81% imekamilika na 19% imebaki kwa ajili ya kutoa matangazo ya watu kuomba kufanya kazi ya kkarani.
Katika zoezi hili ajira zimegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni; Karani wa kuhesabu, Msimamzi wa Maudhui na Karani wa Mfumo (TEHAMA), hivyo imesisitizwa watu wajitokeze kwa wingi kuomba nafasi hizi.
“Asijitokeze muombaji yoyote kutoa fedha ili apatiwe nafasi ya ukarani, hii ni kosa kisheria”, amesema Bi. Makinda.
Bi. Makinda amesisitiza kuwa, itumike mitandao mbalimbali kuweka ujumbe wa Sensa, hotuba mbalimbali za viongozi lazima mwishoni kuwepo na ujumbe wa sensa. Pia katika vipindi vyote vya runinga na redio kuwepo na ujumbe huo kwani ni Agenda ya Kitaifa.
Ifikapo Juni mafunzo juu ya kufanya Sensa yatatolewa, na Ifikapo Julai 27 shule zote zitafungwa hadi Septemba 4 ili kurahisisha zoezi hili.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mheshimiwa Allan Kijazi amesema, malengo ya kufanya sense kwanza ni umuhimu wake katika taifa kwani itasaidia katika mambo kama; kupata takwimu za makazi yote, kufanya tathimini ya makazi ili kutoa huduma bora, kukusanya mapato kwa njia bora, Serikali kuendeleza Miji, kujua mgandamizo wa makazi, kufanya umiliki na mengine mazuri.
Amesema pamoja na haya tujitokeze kuhesabiwa na kutoa ushirikiano katika jambo hili.
Kauli Mbiu ya Sensa kwa Mwaka huu ni: “Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa”.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa